Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hapo Mzee Ruta naye bado hajadondosha picha 10 za wachezaji na maselebriti wa Ulaya kwa mpigo. Huku Myoya naye anahimiza uzalendo, Cole anashusha paraboz kwa "mate" wake...ali mradi raha tupu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
KUTIBU MATATIZO YA UPUNGUFU WA PROTINI

Matatizo ya upungufu wa protini hutibika kwa kula protini kwa wingi. Mtu mwenye tatizo anaweza kula au kulishwa moja kwa moja kupitia mdomo wake kama kawaida, au kama hajiwezi anaweza akalishwa kwa kupitia mipira kama utaratibu maalum wa lishe uitwao Total Parenteral Nutrition (TPN).
 
Watoto wenye kwashakoo, akina mama wajawazito, wazee, wagonjwa, wafanyakazi za kutumia sana misuli na watu wengine wote wenye matatizo ya upungufu wa protini wale sana samaki, nyama, maini, mayai, soya, mboga jamii ya maharage (kunde, njugu, njegere, mbaazi nk), maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa (Mfano mtindi, siagi, jibini nk), mbegu jamii ya karanga (Mfano karanga, korosho, nazi nk), mboga za majani na matunda.
 
MAANDALIZI YA VYAKULA VYA PROTINI

Protini ina tabia ya kuharibiwa na joto. Hakikisha haupiki vyakula vya protini kwa moto mkali sana na kwa muda mrefu, vinginevyo kiasi kikubwa cha protini kitaharibiwa na moto. Pika au kaanga kwa joto la wastani na muda wa wastani ili usije ukaziharibu protini zenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…