Muingiliano kati ya dawa na dawa zingine, magonjwa na vyakula
Nadhani tuliwahi kukujuza muingiliano kati ya dawa na dawa zingine, magonjwa, vyakula na vinywaji.
Bado wagonjwa wengi na baadhi ya dalili za magonjwa na magonjwa hutibiwa bila mgonjwa kufanyiwa vipimo hivyo kukosa uhakika kwa 100% kwamba huo ni ugonjwa gani na umesababishwa na vijidudu gani ambavyo huweza kuuliwa vizuri zaidi na dawa gani.

Usugu wa vijidudu vya magonjwa kwa dawa
Hili ni miongoni mwa matatizo makubwa sana ambayo yameanza kuikabili afya yetu na linakua na kutuathiri kila siku.
Matumizi mabaya ya dawa kama kutokamilisha dozi na kutomeza dawa kwa wakati huchangia sana tatizo hili. Matokeo yake ni kwamba hata mtu akinywa dawa bado haponi ugonjwa wake.
Mapungufu ya dawa zenyewe
Hii hutokea mara chache kutokana na utaratibu mzuri uliopo wa kukagua na kusajili dawa zote zinazotengenezwa na kuingizwa nchini. Kuna tatizo la dawa bandia na dawa ambazo hazina ubora wa kuweza kutibu magonjwa. Ukitumia dawa hizi hautaweza kupona kamwe.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.