Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

0813_isabel-dos-santos_390x22021.jpg
 
Hii ni muhimu sana kuliko hata unavyoweza kufikiria. Sio kupoteza muda au kupoteza pesa, la hasha. Ukirudi hospitali na kupima utapata uhakika kwamba umepona vizuri au bado tatizo lipo kidogo na kujua ufanye nini ili kumalizia.
 
Hii ni kwa wagonjwa wote hata ambao walikuwa na matatizo ya upungufu wa damu, macho, malaria, maambukizi katika njia ya mkojo, sukari kupanda au kushuka, homa ya matumbo nk

Usipofanya hivyo unaweza ugonjwa wako ukakaa ndani kwa ndani huku ukiendelea kuambukiza watu wengine, kuwa sugu, kuendelea kukua na kuharibu sehemu zingine za mwili na kuibuka kwa kasi na kuwa mkali zaidi baadae.
 
Kupata ushauri wa kitaalam wa namna ya kuishi vizuri sasa ili kupona kabisa au kujikinga usisumbuliwe tena na ugonjwa huo
Watu wengi hiki ndo kitu ambacho wamekosa na hawajui kama ni lazima wapate. Afya sio suala la kuumwa na kutibiwa tu, sehemu muhimu zaidi ni kupata ushauri wa kuishi vizuri na kuweza kujikinga dhidi ya magonjwa ili uweze kuishi vizuri. Afya sio vipimo, afya sio dawa, afya sio kulazwa. Afya ni kuishi vizuri bila magonjwa wala kusumbuliwa na tatizo lolote kiakili, kijamiii, kimwili wala kimazingira.
 
Ongea na daktari mwambie akushauri jinsi ya kuwa na afya njema. Mwambie akushauri jinsi ya kuishi bila kukumbwa na magonjwa. Mwambie akushauri jinsi ya kujikinga usikumbwe tena na ugonjwa huo. Mwambie akushauri njia nzuri zaidi za matibabu. Kama ugonjwa ni wa kudumu basi mwambie akushauri jinsi ya kuishi nao vizuri.
 
Baada ya kumaliza dawa zako rudi tena hospitali kwa ajili ya vipimo na ushauri. Hii ndio njia nzuri zaidi ya kuhakikisha umepona kabisa na sasa mwili wako uko vizuri, pamoja na kupata ushauri wa jinsi ya kuishi vizuri na afya njema. Fanya hivyo hivyo na kwa watoto wako pia pamoja na watu wengine ambao unawauguza.
 
Back
Top Bottom