CHF hutumika zaidi maeneo ya kijijini kwa kila mtu au familia kuchangia pesa kiasi kati ya sh 5,000/= hadi sh 15,000/= (ni mpango wa hiari na hutofautiana kati ya maeneo mbalimbali) kwa mwaka. Baada ya hapo mtu au wanafamilia hao hupata matibabu bure.
TIKA hutumika zaidi maeneo ya mijini. Unajiunga na kuweka mwenyewe pesa zako za matibabu katika akaunti yako na utatumia kadi yako kupata matibabu mara tu utakapokuwa unaumwa.
Njia rahisi zaidi ya kupata matibabu mazuri na kwa urahisi ni kujipanga vizuri. Jipange vizuri kwa ajili ya matibabu yako siku zote na muda wote. Pia hakikisha una mawasiliano na usafiri wa uhakika ili ikusaidie ikitokea umepata dharura wakati wa usiku ambapo usafiri wa umma hakuna.