Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1510431122591.jpg
 
WATU FULANI HUDHANI kwamba kulala usingizi ni kupoteza wakati. Wao huwa na shughuli nyingi za kibiashara na kirafiki kila siku, na hulala tu wanapokuwa wachovu sana. Kwa upande mwingine, wengine hutamani sana kupata usingizi mtamu lakini hujigeuza-geuza kitandani hadi asubuhi.
 
Tuendeleapo kuzeeka, mazoea yetu ya kulala hubadilika. Mtoto mchanga hulala kwa vipindi vingi vifupi vyenye jumla ya saa 18 hivi kwa siku. Kulingana na wataalamu wa usingizi, watu fulani wazima wanahitaji kulala kwa muda wa saa tatu tu huku wengine wakihitaji muda wa saa kumi.
 
Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha pia kwamba vijana fulani huona ugumu wa kuamka asubuhi kwa sababu ya mabadiliko ya utendaji wa mwili. Yaonekana mwili wa vijana hubadilika wanapobalehe, na ndiyo sababu wao hutaka kulala usiku sana na kuamka wakiwa wamechelewa.
 
Mazoea hayo ni ya kawaida nayo huendelea hadi miaka ya katikati na ya mwisho ya ujanani
Utendaji wa miili yetu huongozwa na kemikali zilizo mwilini na tayari nyingi zinajulikana. Mojawapo ya kemikali zinazodhaniwa zinasababisha usingizi ni homoni inayoitwa melatonin.
 
Homoni hiyo hutengenezwa kwenye ubongo, na baadhi ya wanasayansi wanaamini kwamba ndiyo inayopunguza utendaji wa mwili kabla tu ya usingizi. Homoni hiyo inapotengenezwa, joto la mwili na damu inayoenda kwenye ubongo hupungua, na pole kwa pole misuli yetu hulegea. Ni nini kinachotukia mtu anapoanza kulala usingizi?
 
Njia Kuu ya Asili Inayoburudisha”
Muda wa saa mbili hivi baada ya kulala usingizi, macho yetu huanza kusogea-sogea haraka. Jambo hilo limewafanya wanasayansi wagawanye usingizi katika vipindi viwili: kipindi cha kusogeza macho haraka na kipindi cha kutosogeza macho.
 
Back
Top Bottom