Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

VVU huweza kuenezwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye virusi hivyo bila kutumia kinga; kwa njia ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, kujifungua au kunyonyesha; na kwa njia ya damu kupitia kwenye sindano za hospitalini, sindano za kawaida au vitu vingine vyenye makali ya kukata au kutoboa.
 
Utoaji wa elimu ya VVU kwa watu wote pamoja na mapambano dhidi ya unyanyapaa na ubaguzi havina budi kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku ikiwa ni pamoja utoaji wa elimu kuhusu uzuiaji na upimaji wa VVU, pamoja na uhudumiaji wa waathirika.
 
Wasichana na wavulana hawana budi kupewa ulinzi sawa katika familia zao, shuleni na kwenye jamii. Endapo ulinzi wa namna hiyo ukikosekana, watoto hukabiliwa na hatari zaidi ya kukumbwa na vurugu, udhalilishwaji kingono, unyonywaji, utumikishwaji
 
tabia chafu pamoja na kubaguliwa. Kuishi pamoja na familia , uandikishaji wa vizazi, upatikanaji wa huduma za msingi, mfumo wa sheria unaozingatia haki za watoto, pamoja na ushiriki wa watoto katika kujijengea maarifa na stadi za kujilinda wenyewe, ni mambo ya msingi katika ujenzi wa mazingira mazuri kwa watoto kwa ajili ya kuendeleza uwezo wao na kufanikisha malengo yao.
 
Back
Top Bottom