Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 sasa amekuwa akilalamikiwa kushuka kiwango, kwani amefunga goli moja tu katika mechi saba La Liga msimu huu, kiwango cha chini kuliko kawaida yake.
 
Akihojiwa na L'Equipe, Ronaldo alisema kwamba hana sababu ya kujibu lolote kuhusu shutuma hizo, lakini amesisitiza kuwa mchango wake kwa timu ni zaidi ya magoli.
 
Unaweza kuniona kama mashine ya magoli, kama mtu anayehitaji kufunga kila wakati. Kama hivyo ndivyo ilivyo, basi kila mtu hatajali kama nimecheza vizuri ama la!.
 
Napimwa kwa kufunga tu, lakini sikubaliani na hilo. Ndio maana naepuka kusoma au kusikiliza yanayosemwa kuhusu mimi.
 
Ronaldo ameanza vizuri michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa idadi ya mabao, ambako amefunga mara sita katika mechi nne za hatua ya makundi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…