Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sababu napendaga magazeti yako ya ufafanuzi full burudani na mifano kuntu. Upo vizuri shimba. Awesome answer
 
Inawezekana hakuwa wa kwangu”, “Yamkini Mungu hakupanga tuwe pamoja”, “Labda Mungu ameniepushia mengi”. Mara kwa mara wengi tumesikia sentensi zinazofanana na hizi hususani kwenye vinywa vya watu, marafiki au ndugu zetu ambao wamewahi kuachana, kutengana au kuvunja mahusiano.
 
Inawezekana hakuwa wa kwangu”, “Yamkini Mungu hakupanga tuwe pamoja”, “Labda Mungu ameniepushia mengi”. Mara kwa mara wengi tumesikia sentensi zinazofanana na hizi hususani kwenye vinywa vya watu, marafiki au ndugu zetu ambao wamewahi kuachana, kutengana au kuvunja mahusiano.
 
Kila mmoja wetu hushangaa na kuchanganyikiwa akifikiria kwa nini mapenzi ambayo yanaonekana kunoga kiasi hiki yanaishia kwenye machungu na majuto kiasi hiki. Kwa nini muda mzuri tuliouwekeza kwenye mioyo ya wapenzi wetu unaishia kupotea kihasara namna hii?
 
Jambo hili huwatatiza wengi sana na yamkini wewe ni mmoja wao. Tafiti za kisaikolojia kwenye eneo la mahusiano pamoja na yale mengi tunayokutana nayo kwenye kuwashauri wapenzi na wanandoa wengi yametufanya kufikia hitimisho kwamba mapenzi huwa yana hatua zake
 
na kwa bahati mbaya wapenzi wengi wanashindwa kuziendea hatua hizo moja baada ya nyingine badala yake wanaishia njiani, kama nilivyosema kwenye utangulizi kwamba wengi huishia hatua ya tatu. Fuatana nami katika makala hii uzielewe vizuri zaidi hatua hizi zitakazokusaidia sana.
 
Kuingia katika penzi

Hii ni hatua ya mwanzoni kabisa wakati umekutana na mtu ambaye unaona kama ni ndoto yako imekuwa dhahiri. Mtu uliyemtamani kwa muda mrefu sana. Hapa unajihisi mwenye furaha kuliko mtu yeyote yule. Hisia zako zote zinatawaliwa na mihemko ya kuwa na huyo unayemfia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…