Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1511117564508.jpg
 
Hapa mwanamke anajihisi salama zaidi ya wakati akiwa hana mtoto na mwanaume anajiona ana jukumu la kuwalinda mama na mtoto. Hisia za kuyapenda majukumu huanza na ulazima wa kujibidisha huongezeka. Mara nyingi furaha na ule umoja inapoongezeka kila mmoja anahisi hakukosea kumpenda mwenzake na kwamba kila mmoja amekuja kwenye maisha ya mwenzake kwa sababu sahihi.
 
Machungu ya kuhisi ulikosea

Katika hali ya kushangaza kabisa, katika kipindi hiki upepo unaanza kubadilika na kama ni safari ya baharini basi mnaanza kuona mawimbi yakivuma kwenye chombo chenu. Ndani yako unaanza kuona yale matumaini uliyokuwa nayo kwenye hatua ya kwanza na ya pili yanaanza kuzama.
 
Kuna vitu zamani ulikuwa ukiviona vidogo tu kwenye tabia za mwenzako, ulikuwa ukiviona kama njiti, sikuhizi unaanza kuviona vikubwa kama misumari, na vinakuchoma kama moto. Vipindi vya hasira, kelele na kufokeana vinaanza kuingia kwenye mahusiano yenu.
 
Ila kwa mbali moyoni mwako au akilini mwako unaweza kuwaza labda iko siku hisi hisia zitaniisha ili nirudi kumpenda tena huyu mume au mke wangu. Katika kipindi hiki wengi wanatoa sentensi za “tuachane kama tumeshindwana”, “kama umenishindwa nirudishe kwetu”, “nikirudi nisikukute” n.k.
 
Kiukweli katika hali na upepo huu ndani yako unahisi kabisa kwamba ulikosea kumchagua yeye, na wengine wanajutia kabisa uamuzi wao wa kuamua kuoana na yeye. Zile hisia za kumpenda, kumlinda, kumfurahisha na kumtetea mpenzi wako zinaenda na maji mbali kabisa, tena hutaki kabisa kumsikia, unatamani hata asirudi nyumbani kwa jinsi anavyokuudhi.
 
Kama mwanzoni mlikuwa mnafurahia tendo la ndoa basi sasa ndio tendo hilo linaingia shubiri. Hutaki akuguse wala akusogelee. Kwa bahati mbaya vita hii na kutofautiana huku kunapozidi uwezekano wa michepuko huongezeka ambayo na hiyo huongeza vita na mchimbiko pale ambapo kunakugundulika.
 
Katika kipindi hiki kiu ya kuwa pamoja imekufa na kuzikwa kabisa, wengine wanatafuta maeneo ya kupumulia ilimradi asiwe nyumbani, wakushinda baa ndio anapotelea huko kabisa, wakushinda kazini ndio atakaa huko hadi usiku wa manane kama vile mfanyakazi bora kumbe ana maumivu, wakushinda makanisani basi ndiyo utadhani kaambiwa Yesu anarudi kesho kumbe anamkimbia mwenza wake. Yaani kushoto na kulia kote kunakuwa shubiri.
 
Back
Top Bottom