Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MAN UTD KUJARIBU TENA KUMSAJILI OBERLIN


Manchester United hawajakata tamaa kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Dimitri Oberlin, kwa mujibu wa habari kutoka TuttoMercatoWeb .
Mchezaji huyo wa miaka 20 ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo FC Basel, inaaminika kuwa aliwahi kukataa fursa hiyo, lakini miamba wa Old Trafford wanajipanga kutoa euro milioni 5 kumnunua.
 
MAN CITY HUENDA WAKAMPOTEZA KINDA WAO KWA LIVERPOOL


Liverpool wana tumaini la kumsajili kinda mahiri wa Manchester City Javairo Dilrosun, kwa mujibu wa ESPN .
City walikuwa na tumaini kubwa kubaki na kinda huyo wa miaka 19 baada ya kumpoteza Jadon Sancho aliyetimkia Dortmund majira ya joto, lakini Juventus, RB Leipzig na Valencia pia zinatamani huduma yake,
 
ARSENAL YAPANGA KUZUNGUMZA NA GORETZKA


Arsenal wataanza mjadala na kiungo wa Schalke Leon Goretzka mwaka mpya kwani wanajiandaa na maisha bila ya Mesut Ozi, kwa mujibu wa Daily Mail .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani atakuwa mchezaij huru ifikapo 2018 na ataruhusiwa kuongea na klabu nyingine kuanzia Januari.
 
1511346408281.jpg
 
MAN UTD NA ARSENAL ZAMWANIA PEREIRA


Manchester United na Arsenal zinamfukuzia kiungo wa Porto Danilo Pereira, limedai gazeti la The Sun .
Klabu zote zimemtupia jicho mshindi huyo wa Euro 2016 na kumekuwa na habari chanya kuwa amerudisha majibu Old Trafford na Emirates.
 
BARCA YATENGA €20M KUMSAJILI OZIL


Barcelona wanaamini ofa ya €20 milion itatosha kumsajili Mesut Ozil kutoka Arsena dirisha la uhamisho Januari, Mundo Deportivo limeripoti.
Miamba hao wa Catalan wanataka kumsajili kiungo huyo wa Kijerumani ikiwa wataikosa saini ya Philippe Coutinho.
 
MKHITARYAN APIGANIA MUSTAKABALI WAKE MAN UTD


Henrikh Mkhitaryan anapambana na hali yake kuokoa kibarua chake Manchester United baada ya kuwa katika kiwango duni siku za hivi karibuni The Sun .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Armenia alifurahia mwanzo mzuri msimu huu, lakini amekuwa na kiwango duni mwishoni na aliachwa kwenye kikosi kilichoshinda 4-1 dhidi ya Newcastle.
 
DE GEA BADO ANATAKIWA MADRID


Kipa wa Manchester United David de Gea bado ni shabaha nambari moja kwa Real Madrid usajili wa majira ya joto, kwa mujibu wa Cadena SER .
Madrid wanayo nafasi kubwa kumsajili Kepa Arrizabalaga, lakini wanataka kutoa euro milioni 70 kwa ajili ya De Gea kuliko euro milioni 50 kwa ajili ya kipa wa Athletic Bilbao.
 
Ni jambo la kawaida kuona kiongozi wa nchi za Afrika akitawala kwa zaidi ya miaka 30 huku aking’ang’ania kuendelea kuwa madarakani, hata kama wananchi wake hawamtaki au afya yake hairuhusu.

Viongozi wengi wanaong’ang’ania madarakani ni wale walioongoza mapambano ya kupigania uhuru wa nchi zao au kuongoza vita vya msituni na kufanya mapinduzi.
 
Fikra zao zinawaambia kwamba wao ndiyo wenye hatimiliki ya nchi zao na wanatakiwa kutawala daima.

Chemchemi ya mabadiliko imeanza kuwakumba viongozi wa namna hiyo na tumeshuhudia viongozi kadhaa wa Kaskazini na Magharibi mwa Afrika wakiondolewa ama kwa nguvu kutoka nje au ndani ya nchi zao.
 
Vuguvugu la mabadiliko katika nchi za Misri, Tunisia na Libya (Arab Spring) halikuwaacha salama. Viongozi wa muda mrefu wa mataifa hayo; Hosni Mubaraki, Zine el Abidine Ben Ali na Muammar Gaddafi ama walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa au kuuawa.
 
Back
Top Bottom