Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1511345744245.jpg
 
Baada ya Zimbabwe kupata uhuru wake mwaka 1980, Mugabe alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mzawa. Alipokea kijiti kutoka kwa Ian Smith ambaye aliongoza Serikali ya Rhodesia ambayo sasa inatambulika kama Zimbabwe.

Katika kipindi chote cha utawala wake, Mugabe alifanikiwa kujenga umoja wa kitaifa na kuimarisha uchumi wa Taifa hilo.
 
Hata hivyo, uchumi wa nchi hiyo ulianza kudorora miaka ya 2000 baada ya kiongozi huyo kuwafukuza wazungu ambao walikuwa wamewekeza kwenye kilimo.

Hali ya maisha ya Wazimbabwe ilikuwa mbaya, thamani ya dola ya Zimbabwe iliporomoka zaidi na kupoteza thamani yake. Mpaka sasa nchi hiyo inatumia sarafu za nchi nyingine kama vile Dola ya Marekani, Randi ya Afrika Kusini, Rupia ya India Paundi ya Uingereza na Pula ya Botswana.
 
Licha ya kuwanyang’anya mashamba wazungu na kuwamilikisha wazawa, bado hali ya uchumi wa Zimbabwe haijasimama kama awali ikithibitisha kwamba wawekezaji waliofukuzwa walikuwa wameshikilia sehemu ya uchumi wa nchi hiyo.

Pamoja na msukosuko wa kiuchumi, Mugabe amefanya kazi kubwa ambayo imemjengea heshima kwa Wazimbabwe. Hata hivyo, anaweza kupoteza heshima hiyo kama hatasoma alama za nyakati na kubaini wananchi wake wanataka nini.
 
Zimbabwe ni nchi yenye watu milioni 16.5, ina wasomi wengi wenye uwezo na kuiongoza. Sasa ni wakati wa Mugabe kuona mahitaji ya watu wake ambao wanataka kiongozi mpya mwenye mawazo mapya ya kuiongoza.

Mbinu ya kutaka kumrithisha madaraka mke wake, Grace baada ya kumfukuza makamu wake Emmerson Mnangagwa imeliamsha jeshi la nchi hiyo na kuona haja ya kumwondoa kiongozi huyo kwa amani na kusimika kiongozi mwingine ambaye atachukua nafasi ya Mugabe.
 
Back
Top Bottom