Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tiba ya pumu huwa inagawanywa kwenye makundi mawili; tiba ya kutoa msaada wa haraka na tiba ya muda mrefu ya kudhibiti pumu. Tiba ya kutoa msaada wa haraka ni ile inayotolewa pale mgonjwa anapoona dalili za kubanwa pumu na tiba ya muda mrefu ya kudhibiti pumu inalenga kupunguza athari zinazotokea kwenye njia za hewa na hivyo kuzuia kutokea kwa kubanwa na pumu.
 
Dawa za pumu huweza kutolewa kama vidonge, lakini nyingi huwa kama unga au mvuke ambavyo mgonjwa atavitumia kupitia kinywani mwake kwa kutumia kifaa kinachoitwa Inhaler. Inhaler ni kifaa kinavyosaidia dawa kupita kirahisi katika njia za hewa kuelekea kwenye mapafu.
 
Tiba Ya Pumu Ya Kutoa Msaada Wa Haraka

Mgonjwa ye yote wa pumu lazima awe na njia ya kupata msaada wa haraka ili kuzuia tatizo lisiwe kubwa pale anapohisi dalili za kubanwa na pumu. Chaguo la kwanza kwa mgonjwa wa pumu la kupata msaada pale anapoanza kujihisi vibaya ni Inhaled short-acting beta2-agonists.
 
Hizi ni dawa ambazo mtumiaji atazipata kupitia kifaa kinachoitwa Inhaler. Dawa hizi hufanya kazi haraka sana na kulegeza misuli ya njia ya hewa iliyokaza pale mgonjwa anapobanwa na pumu na hivyo kufungua njia ya hewa. Vifaa hiivi vipo vya aina tofauti, yafaa kumwuliza daktari wako kuhusu njia nzuri ya kukitumia kifaa ulicho nacho.
 
Mgonjwa anatakiwa kutumia inhaler mara tu anapoanza kusikia dalili za kubanwa na pumu, hivyo basi mgonjwa anashauriwa kuwa na kifaa chake po pote alipo. Kifaa hiki kinashauriwa kisitumike zaidi ya mara mbili kwa wiki, endapo matumizi yanaanza kuzidi idadi hiyo ni vizuri mgonjwa amwambie daktari wake kuhusu hali yake ili aweze kubadilishiwa mpango wake wa kuudhibiti ugonjwa wa pumu. Kifaa hiki hata hivyo hakipunguzi tatizo la kuathirika kwa njia za hewa kama tutakavyoona katika tiba ya muda mrefu ya kudhibiti pumu.
 
Tiba Ya Muda Mrefu Ya Kudhibiti Pumu

Watu wengi wenye pumu hutumia njia za muda mrefu za kudhibiti pumu kila siku ili kuzuia uwezekano wa kutokea matatizo yanayoambatana na ugonjwa huo. Njia hizi za muda mrefu hupunguza kuathirika kwa njia za hewa (kuvimba kwa ndani na kuwa sikivu kuzidi kiwango) na hivyo kuondoa uwezekano wa kutokea kwa kubanwa na pumu. Njia hizi hazisaidii kutoa msaada wa haraka kwa mgonjwa.
 
Watu wengi wenye pumu hutumia corticosteroids ( inhaled corticosteroids ) kila siku ili kudhibiti ugonjwa wa pumu walio nao. Corticosteroids ni kundi la kemikali ambazo hutengenezwa na figo au kwenye maabara ambazo hufanya kazi nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na kupunguza vimbe katika mwili
 
Matumizi ya dawa hii yameonyesha kuwa bora katika kuzuia kutokea kwa uvimbe na athari nyingine kwenye njia za hewa zinazotokana na mtu kuvuta hewa yenye vitu visivyopendwa na mwili wa muathirika. Dawa hii hutumiwa kwa kuvutwa kwa mdomo kutoka kwenye kifaa maalumu.
 
Matumizi ya inhaled corticosteroids yana athari zake zikiwa ni pamoja na maambukizi ya mdomoni (thrush) yanayosabababishwa na matone ya dawa hiyo kuangukia kwenye mdomo au kooni. Dawa hiyo pia huweza kuathiri mboni za macho na kupunguza uimara wa mifupa endapo itatumika kwa muda mrefu.
 
Peak Flow Meter

Hiki ni kifaa kidogo cha kushikwa mkononi ambacho kinaonyesha jinsi hewa inavyotoka kutoka katika mapafu ya mtumiaji. Mtumiaji anapuliza kwa mdomo kwenye kifaa hicho na ataonyeshwa alama alizopata ( peak flow number) ambazo ni ishara ya ubora wa kiafya wa mapafu yake kwa wakati huo alipopuliza kwenye kifaa hicho.
 
Mtumiaji anakitumia kifaa hicho kwa namna na muda alioshauriwa na daktari wake, kwa mfano, daktari anaweza kumshauri mgonjwa kukitumia kifaa hichio kila siku asubuhi na kunukuu alama anazopata kisha kumpelekea baada ya kipindi fulani ili aweze
kushauriwa dawa za kuendelea kuzitumia.
 
453f5382560aa925139a50bf2fd24687.jpg
 
Back
Top Bottom