Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Gout ni ugonjwa ambao umefahamika kwa miaka mingi sana. Inasadikika kuwa watu wa kwanza kuutambua ugonjwa huu walikuwa watu wa Misri, kunako miaka ya 2640BC. Mtaalamu wao wa tiba Hippocrates aliuita ugonjwa huu “Ugonjwa Wa Kumfanya Mtu Asitembee” na aliuhusisha ugonjwa huu na namna ya mtu anavyoishi
 
Hadi hivi leo ugonjwa huu ni tatizo la jamii nyingi, ambao huwapa maumivu makali sana wale ambao wameathirika. Kwa bahati nzuri ugonjwa huu hutibika na kuna hatua za kuchukua zinazoeleweka ili usipatwe na ugonjwa huu. Katika ukurasa huu tutatazama ugonjwa wa gout ni nini , chanzo cha ugonjwa wa gout, dalili zake na namna ya kuutibu pale unapokuwa umeathirika.
 
Gout Ni Nini?



Gout ni namna moja ya Arthritis, ugonjwa ambao hushambulia joints (sehemu za maungio ya mifupa). Huu ndio ugonjwa wa joints ambao huwashambulia sana na kuwapa maumivu makali wanaume. Wanawake pia huweza kuathirika na ugonjwa huu hasa baada ya kukoma hedhi.
 
Ugonjwa huu huleta maumivu makali ya ghafla, hasa kwenye sehemu linapoanzia dole gumba la mguu. Dalili za ugonjwa huanza kuonekana pale uric acid, tindikali ambayo huzalishwa na mwili katika ufanyaji kazi wake (ambayo haina manufaa kwa mwili) inapobakia katika viungo vya mwili na katika majimaji ya mwili.
 
Uric acid iliyoganda (tophi) huweza kujikusanya na kubaki chini ya ngozi inayozunguka joints, huweza pia kujikusanya ndani ya figo na kusababisha kidney stones (namna ya kokoto ndogo ndani ya figo).
 
Gout inaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye maungio ya mifupa na figo. Endapo hatua za kuutibu ugonjwa huu hazitachukuliwa kwa muda mrefu (miaka 10 au zaidi), madhara ya kudumu humtokea mgonjwa.
 
Chanzo Cha Gout Ni Nini?



Gout kutokea kimsingi pale tindikali aina ya uric (uric acid) inapozidi kiwango katika mwili wa binadamu hali ambayo kiutaalamu huitwa hyperuricemia. Tindikali hii ni matokeo ya kuvunjwavunjwa na mwili kwa aina fulani za chakula kama nyama, nyama ya kuku na chakula cha baharini.
 
Tindikali hii kwa kawaida huchanganyika na damu na mwisho hutolewa nje ya mwili pamoja na mkojo kupitia figo. Tindikali hii ikitengenezwa kwa wingi mno au isipotolewa nje ya mwili kwa kiwango kinachosatahili, ile inayobakia huganda na kukaa kwenye maeneo ya joints na kusababisha maumivu kwenye joints hizo na maeneo yaliyo karibu. Kuna mazingira ambayo hupelekea hali hii ya uzidifu wa tindikali ya uric katika mwili na mwishowe gout kutokea nayo ni:
 
Mtindo wa maisha: Unywaji wa pombe huzuia utolewaji wa uric acid nje ya mwili na ulaji wa chakula chenye purine kwa wingi husababisha kiwango cha tindikali ya uric kuwa kikubwa mwilini.
 
Back
Top Bottom