Mwanajiolojia mkuu Gudmundur Omar Fridleifsson, wa kampuni ya nishati ya HS Orka anasema: "Joto linaendelea kuongezeka, lakini tunaendelea kuchimba kwenye mawe hayo moto. Nikisema mawe moto, narejelea mawe yenye kiwango cha joto cha 400 hadi 500C."
Wakifikia kina cha kilomita 5, wanatarajia kupata mawe yaliyoyeyuka ambayo yamechanganyika na maji.
Mchanganyiko huo una kiwango cha juu sana cha nishati.
Bw Margeirsson anasema hilo likifanikiwa, basi lina maana kwamba wataweza kuchimba visima vichache na kupata kiwango cha juu sana cha nishati na hivyo kutoharibu mazingira sana kwa kuchimba visima vya kawi ya mvuke.
Mwaka 2009, kundi jingine lilijaribu kuchimba kwenye volkano lakini walipofikia kina cha 2,100m wakakumbana na mawe yaliyoyeyuka na wakashindwa kuendelea.
Viumbe wote hai huhitaji chakula ili kuishi. Chakula huwapa binadamu nguvu ili waweze kufanya shughuli zao za kila siku, huwawezesha kujenga na kuikarabati miili yao, na huwawezesha kupambana na maradhi mbalimbali.
Ili mwili uweze kuyafanya yote hayo na kuwa na afya nzuri, inabidi upate chakula cha aina mbalimbali. Mada ya leo inahusu umuhimu wa virutubishi katika mwili wa binadamu ambapo tutavitaja virutubishi hivyo na kuelezea umuhimu wa kila kimoja.