Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SIMEONE ANATAKA KUMSAJILI PASTORE

Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone anataka kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain Javier Pastore katika dirisha la uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa AS .
Pastore hana furaha katika klabu ya PSG na pia anatakiwa na Inter Milan, lakini Simeone anaamini ataweza kumshawishi Mwargentina mwenzake kuhamia Hispania mwaka mpya.
 
RONALDO AANZA MAZUNGUMZO NA PSG

Cristiano Ronaldo amemwambia wakala wake Jorge Mendes kuanza mazungumzo na Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa DiarioGol .
Inadaiwa kuwa Mreno huyo anataka aidha kuongezewa ujira Real Madrid au kuondoka mwishoni mwa msimu huu, ombi ambalo rais Florentino Perez hana mpango wa kulifanyia kazi.
 
DORTMUND WANAMTAKA MKHITARYAN

Borussia Dortmund wanatamani kumrejesha mshambuliaji wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan klabuni mwao, kwa mujibu wa BBC .
Mkhitaryan aliondoka Dortmund kwenda United kwa dau la paundi milioni 30 majira ya joto 2016, lakini amepata wakati mgumu kuonyesha uwezo wake Old Trafford.
Jose Mourinho amemlaumu Mkhitaryan kwa kupotea mchezoni na sasa Dortmund wanataka kumsajili tena Mwarmenia huyo.
 
CAN AKUBALI MASHARTI KUJIUNGA NA JUVENTUS

Kiungo wa Liverpool Emre Can amekubali masharti ya binafsi baina yake na mabingwa Serie A Juventus, kwa mujibu wa Tuttosport .
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ujerumani atakuwa amemaliza mkataba wake mwisho wa msimu wa 2017-18, na mazungumzo ya mkataba mpya yamesimama kwa mujibu wa habari. Can ataweza kusani mkataba wa awali na Juventus Januari.
 
ARSENAL ZINAMTAKA LIVERPOOL DRAXLER

Arsenal wameungana na Liverpool katika mbio za kuiwania saini ya Julian Draxler kutoka Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa The Mirror .
Inafahamika kuwa Liverpool wanamhusudu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani na wanataka kumsajli kwa mkopo, lakini PSG wapo tayari kumuuza.
 
SHAW MBIONI KUONDOKA UNITED KWA MKOPO

Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw anajipanga kujiunga na Newcastle kwa mkopo kwa mujibu wa habari kutoka the Daily Mirror .
 
PSG YAIPIKU MAN CITY MBIO ZA ALEXIS

Paris Saint-Germain inaitangulia Manchester City katika mbio za kumfukuzia nyota wa Arsenal Alexis Sanchez Januari, The Mirror limeripoti.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile unafikia ukomo mwisho wa msimu huu, na PSG imeripotiwa kuwa kwenye mchakato wa kumsajli kwa mkataba wa awali wanapojipanga kumruhusu Neymar kwenda Real Madrid msimu ujao wa majira ya joto.
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 aliteuliwa kuwa nahodha wa klabu kufuatia kuondoka kwa Wayne Rooney wakati wa majira ya joto, lakini ushinda dhidi ya Burton Albion kwenye kombe la EFL ndiyo mechi pekee ya kimashindano ambayo Carrick alivaa kitambaa cha ukapteni.
Carrick alifafanua Ijumaa iliyopita kuwa kutokuwepo kwake kutokana na matatizo ya moyo , lakini nyota huyo anaendelea vizuri na Mourinho amethibitisha kuwa kuna nafasi katika klabu kwa ajili yake hata baada ya kuachana na mpira.
"Michael kama mtu ni muhimu zaidi kuliko Michael kama mchezaji. Hivyo tutampa muda wa kupumzika, kupona na kutafakari. Kwa kufanya uamuzi kama anataka kuendelea kucheza, au anataka kuacha," aliwaambia waandishi wa habari.
"Anajua kwamba kwenye ofisi yangu kuna kiti kwa ajili yake ikiwa anataka, kama anataka. Kiti chake kipo pale ofisini .Nataka hivyo, bodi nayo inataka hivyo , wamiliki wanataka hivyo.
"Lakini anataka kuwa mchezaji hadi mwisho wa msimu na sasa anajisikia vizuri kurejea kwenye mazoezi. Chaguo moja zaidi kwetu.Tunahitaji wachezaji na ikiwa Michael atataka, nitafurahi na hilo."
Carrick alijiunga na United mwaka 2006 na amecheza michezo 460 katika klabu kwenye mashindano yote.
 
Inafahamika kuwa ofa ya washika mtutu wa London ya £90m ilikataliwa na Monaco kwa ajili ya Mfaransa huyo katika dirisha la uhamisho wa majira ya joto, kadhalika Liverpool nao wanaaminika kuvutiwa na mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa Daily Mail, miamba hao wa London Kaskazini watarejea tena Januari kwa ajili ya mchezaji huyo lakini hawatatoa ofa kubwa kama walivyofanya majira ya joto.
Ripoti zinadai kuwa Arsene Wenger ana shauku kubwa ya kuleta mchezaji mahiri katika safu ya mashambulizi kikosini mwake ikiwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez wataondoka klabuni hapo mwakani.
Lemar, ambaye amejiunga na Monaco 2015 kutoka Caen, amecheza mechi 103 kwa miamba hao wa Ligue 1, akifunga magoli 20 na kutoa pasi 25 za goli.
 
Klabu ya Yanga jana imemsainisha mkataba wa miaka miwili, beki wa kati raia wa Kongo, Fiston 'Festo' Kayembe Kanku ambaye alikuwa kwenye majaribio katika timu hiyo kwa muda mrefu.
Usajili huo unakuja siku moja baada ya safu ya ulinzi ya Yanga kuruhusu bao la tano katika Ligi Kuu Bara jana wakilazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Usajili wa Kayembe unazima kabisa uwezekano wa beki Mtogo, Vincent Bossou kurejeshwa Jangwani, licha ya kupigiwa debe na wadau mbalimbali wa klabu hiyo, arejeshwe kikosini.
Inasadikika kuwa hali mbaya ya kiuchumi ilisababisha Yanga kutompa mkataba mpya Bossou, lakini kitendo cha klabu kumsajili Kayembe anayetokea Balende FC ya kwao, Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo (DRC) kinaashiria imeamua kuachana na Mtogo huyo moja kwa moja.
Kupitia ukurasa wao wa Instragram, Yanga wameandika ujumbe huu: “Fiston 'Festo' Kayembe Kanku amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na [HASHTAG]#mabingwamara27[/HASHTAG] @yangasc akitokea Balende Fc ya DR CONGO.
 
Umeupitia Uzi wa harry porter wa Sky?
 
0276bfb2d2482d60797b315357194e04.jpg
 
Back
Top Bottom