Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-12-02-22-29-01.png
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Edda Sanga, baadhi ya tafiti zinaeleza asilimia 35 ya wanaume wanapigwa na wake zao ingawa hawasemi kutokana na kuona aibu kwa sababu bado mtazamo wa jamii umeegemea kwenye mfumo dume ambao unampa mwanaume nguvu ya kumtawala mwanamke.
 
Baya zaidi katika unyanyasaji huu ni ubakaji dhidi ya wanaume, jambo ambalo wanaume wengi hulinyamazia kimya kwa kuhofia kudhalilika.
 
Tukiendelea kuadhimisha siku hizi 16 za muhimu za unyanyasaji, ni vizuri kuwaangazia wanawake na mabinti lakini si salama sana kuwaacha nyuma akina baba na watoto wa kiume.
 
Ndiyo maana tunasisitiza nguvu za kampeni, makongamano, elimu na uhamasishaji, zielekezwe na kwa wanaume pia. Ikiwezekana, tuanze kutengeneza vipeperushi kuwahamasisha waripoti, pindi wanapofanyiwa ukatili kama huu wa kubakwa.
 
Takwimu zinasema, mwanamke mmoja kati ya wanne hunyanyaswa kijinsia na mwanaume mmoja kati ya saba, hunyanyaswa pia. Niliwahi kufanya mahojiano na Adolphina Chialo wakati huo akiwa ni Naibu Kamishna Mkuu wa Polisi,
 
alisema wanapokea kesi za wanaume kunyanyasika hasa pindi kipato kinaposhuka au wakiwa hawana kazi. Ni wakati wenu wanaume kujiweka wazi na kueleza madhila yenu ili yatafutiwe ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom