Lakini tukumbuke kuwa wanaume au watoto wa kiume, nao wananyanyasika. Mwanaume akipigwa na mke wake au mwenza wake, akitukanwa au akifanyiwa aina yoyote ile inayoweza kuitwa ni unyanyasaji, basi huo nao ni ukatili wa kijinsia.
Hivyo basi, wakati tunapoadhimisha siku hii ni vyema kama tutaanza kuwaangazia akina baba na watoto wa kiume ambao kimsingi wanakutana na aina tofauti za unyanyasaji.
Kwa mfano, kama wanaume wanalaumiwa kwa kurubuni mabinti au kuwabaka, vivyo hivyo, wapo watoto wa kiume wanaorubuniwa na wanawake wenye umri mkubwa kushirikiana nao vitendo vya ngono.
Hivyo basi, tunapoangalia madhara ya unyanyasaji huo, tukumbuke kuwa kama vitendo hivyo vinamuathari mwanamke au mtoto wa kike, ikiwamo mimba, maradhi na kuathirika kisaikolojia, hali kadhalika mwanaume huathirika kwa namna yake.
Kampeni hii ya kimataifa ilianzishwa kwa mara ya kwanza na taasisi ya Kidunia ya Uongozi wa Wanawake, iliyoratibiwa na Kituo cha Uongozi wa Kidunia wa wanawake mwaka 1991.
Kwa kuwa Siku 16 za kupinga ukatili huu zinatukumbusha kujitathmini, kupaza sauti zetu,
kulindana na serikali kuongeza juhudi katika kupambana na ukatili, lakini wasiwasi wangu tunawaacha nyuma wanaume katika hili. Tunadhani hawaathiriki.
Kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema, tusiache yeyote nyuma, basi itapendeza kama hatutawaacha nyuma wanaume pia. Wanaume wasaidiwe kwa kupatiwa elimu, kuhamasishwa na waambiwe wasikae kimya. Wazungume na wafichue pale wanaponyanyasika.
Kama wanapigwa waseme, kama wananyimwa unyumba kwa sababu hawana fedha pia waseme ili wasaidiwe, lakini pia kama wananyanyaswa na mabosi wao maofisini waseme pia.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.