Arsenal walirejea mchezoni kupitia goli la Lacazette ikiwa ni dakika nne tu tangu kuanza kipindi cha pili, Mfaransa huyo akiuzamisha wavuni mpira baada ya kupokea pasi kutoka kwa Aaron Ramsey.
Lingard alifanya jaribio la kushtukiza lakini shuti lake liligongana na Cech na kugonga mwamba kabla ya De Gea kuokoa mashuti mawili hatari kutoka kwa Lacazette na Sanchez.
United walipata goli moja baada ya saa moja tu ya mchezo, Pogba akimzidi nguvu Laurent Koscielny kabla ya kumpasia Lingard ambaye aliunganisha mpira wavuni.
Usiku wa Pogba ulikoma dakika 11 baadaye, kwani kiungo huyo alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga mguuni Bellerin - Hata hivyo Arsenal hawakuweza kutumia mapungufu ya United waliokuwa 10 dimbani.
Manchester United Waliiadhibu safu ya ulinzi ya Arsenal na kuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika uwanja wa Emirates tangu mwezi Januari katika mojawapo ya mechi za ligi ya Uingereza msimu huu.
Kikosi cha Jose Mourinho kilipunguzwa na kuwa na wachezaji 10 katika dakika za mwisho baada ya Paul Pogba kupewa kadi nyekundu kwa kucheza visivyo na walisaidiwa na kipa wao David de Gea katika mechi yote.
Lakini licha ya hayo Arsenal iliadhibiwa mapema na Antonio Valencia wakati alipopata pasi mbaya ilioandaliwa na beki wa Arsenal Koscielny na kuweza kuiweka kifua mbele Manchester United kabla ya Jesse Lingard kufunga la pili baada ya kumpkoonya mpira Shkodran Mustafi.
Kabla ya Pogba kupewa kadi nyekundi alimshinda nguvu Koscielny na kumpatia pasi Lingaard ambaye alifunga bao la tatu na kuipatia United ushindi huo.
Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Pittsburgh cha Pennsylvania nchini Marekani mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka huu, unaonyesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya mitandao ya jamii yanaweza kusababisha magonjwa ya akili, ukiwamo msongo wa mawazo na wasiwasi
Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Pittsburgh cha Pennsylvania nchini Marekani mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka huu, unaonyesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya mitandao ya jamii yanaweza kusababisha magonjwa ya akili, ukiwamo msongo wa mawazo na wasiwasi
Wakati kukiwa na tatizo hilo, inakadiriwa kuwa asilimia 71 ya vijana duniani kote hutembelea mitandao tofauti ya jamii kila siku huku simu za mikononi zinazowezesha kupatikana mitandao hiyo kirahisi zikizidi kubuniwa na kuboreshwa.
Njia hii ni mahususi kwa simu za android pekee, kwani ukifanya hivi katika simu nyingine haitafaa.
1.Zima simu yako
2.Bonyeza kwa pamoja kitufe cha kuwashia simu (Power Button) na kitufe cha juu cha kuongezea sauti (Volume Up Button) kwa sekunde 5 hadi uone simu inawaka.
3.Kwa watumiaji wa simu za Samsung Galaxy bonyeza kwa pamoja kitufe cha kuwashia simu (Power Button) na kitufe cha juu cha kuongezea sauti na Home button.
4.Utaona maandishi madogo upande wa kushoto yaliyopangwa kushuka chini.
Watu wengi wamekuwa hawafahamu wafanyaje ili kutunza betri la simu ambayo ni jipya ili lisiwahi kuaribika. Kama wewe ni miongoni mwa watu hao nakusihi uweze kuambatana nami kwani nitakueleza namna ya kuchaji betri likiwa jipya ili lisiharibike mapema.