Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alisema kama vibali vitathibitika kuwa ni halali, serikali itaanza kuwasaka waliovitoa na kuwafikisha kwenye vyombo vya uchunguzi kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na pia polisi ili hatua zaidi za kisheria zifuate.
 
Tunashirikiana na Takukuru na Polisi kwa sababu kwenye utoaji wa vibali hivyo kuna harufu ya rushwa, huwezi kutoa kibali mtu ajenge sehemu ambayo imekatazwa kisheria, hivyo tukimbaini kiongozi aliyetoa kibali anakabidhiwa Takukuru ili akajieleze huko,” alisema Heche.
 
Aidha, Heche alisema Sheria ya Ardhi, Sheria ya Mipango Miji, Sheria ya Mazingira na Sera ya Ardhi, kwa pamoja zinazungumzia ulinzi wa fukwe za bahari na mito na hivyo, uvamizi huo hauwezi kukubalika katika serikali ya sasa ya awamu ya tano.
 
Naibu Waziri Lugola alisema ni vyema wamiliki wakiwamo wenye nyumba (zikiwamo za kifahari) na majengo mengine kubomoa wenyewe ikiwa wamo ndani ya mita 60 za fukwe kinyume cha sheria kabla serikali haijaanza kuyabomoa.
 
Lugola alieleza hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Wilaya ya Kigamboni na kushuhudia kiasi kikubwa cha uvamizi katika maeneo ya fukwe,
 
ikiwamo ya Kasa maarufu kwa jina la Kidagaa, Mtaa wa Mikenge Kata ya Kimbiji. Alikuta eneo hilo likiwa limejengwa nyumba na kuta kinyume cha sheria na taratibu za uhifadhi wa mazingira.
 
Kwa mujibu wa Lugola, ujenzi aina hiyo wa ndani ya mita 60 za fukwe na kandoni mwa mito ni kinyume cha Sheria ya Mazingira Namba 20 ya mwaka 2004, ambayo inasisitiza kuwa ni kosa kuwapo kwa shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 katika vyanzo vya maji.
 
Back
Top Bottom