Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mara tu baada ya kununu simu. Iwashe simu hiyo kisha angalia ina asilimia ngapi ya chaji. Baada ya kuona ina asilimia ngapi, unashauriwa kufanya yafutayo;
 
Kama ina asilimia hamsini (50%) au zaidi usiweke simu kwenye chaji bali unatakiwa kuitumia, mpaka chaji hiyo itakofika asilimia kumi (10%) ndipo uiweke kwenye chaji.
 
Mara baada ya kuweka kwenye chaji hakikisha unaichaji simu hiyo kwa muda wa masaa matatu ndipo uanze kuitumia tena. Kwani baada ya masaa matatu itakuwa imejaa vizuri kwa ajili ya matumizi.
 
Lakini endapo umenunua simu mpya au betri jipya mara tu baada ya kuwasha ukakuta ina chaji ambayo ina asilimia arobaini na tisa (49%) kushukua chini (49%-0%) tafadhari sana usiitumie simu au betri hilo, bali iweke chaji kwa muda wa masaa matatu ndipo uanze kuitumia simu hiyo.
 
Lakini jambo la muhimu na lakuzingatia ni kwamba kumbuka kuichaji simu yako kila wakati kila inafika chaji kwa kiwango cha asilimia kumi (10%)

Kufanya hivi kutakusaidia sana kuweza kulitunza betri lisiwahi kuaribika mapema.
 
Kiama tishio la bomoabomoa nyumba za kifahari ufukweni
NI kiama! Wamiliki wa nyumba za kifahari na majengo mengine yaliyopo ndani ya vipimo vya umbali wa mita 60 kutoka fukwe za bahari wapo katika tishio la kukumbana na bomoabomoa ya aina yake.
 
Tishio la bomoabomoa hiyo, ambayo haikutajwa ni lini hasa itaanza, linatokana na taarifa iliyotolewa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na pia Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola
 
Aidha, tayari baadhi ya maeneo yameshaanza kukumbana na bomoabomoa hiyo ambayo lengo lake ni kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa na kila mmoja katika uhifadhi wa mazingira.
 
Aidha, tayari baadhi ya maeneo yameshaanza kukumbana na bomoabomoa hiyo ambayo lengo lake ni kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa na kila mmoja katika uhifadhi wa mazingira.
 
Mwishoni mwa wiki, Nipashe ilithibitishiwa na NEMC juu ya kuwapo kwa tangazo la kuwapo kwa bomoabomoa kwa watu wote waliojimilikisha kingo za mito na fukwe za bahari, ikiwamo katika maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini.
 
Akielezea jambo hilo wakati akizungumza na Nipashe, Mwanasheria wa NEMC, John Heche, alisema kuwa fukwe nyingi, zikiwamo karibu zote za Kigamboni jijini Dar es Salaam, tayari zimevamiwa na watu binafsi na kujengwa uzio na majengo mbalimbali, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Mazingira inayolinda fukwe.
 
Heche alisema ingawa baadhi ya wamiliki hudai kuwa wana vibali halali vya kuwaruhusu kujenga, lakini nao wako hatarini kubomolewa kwa sababu kuwapo kwa nyumba au jengo lolote ndani ya ya mita 60 za ufukweni mwa bahari ni kinyume cha sheria, bila kujali kuwa wahusika walipewa vibali na mamlaka yoyote ile.
 
Ufukwe wote wa Kigamboni umehodhiwa na kwa sasa hakuna mwananchi wa kawaida anayeweza kwenda ufukweni…sheria inakataza walichofanya, hivyo wajue kuwa wakati wowote wanaweza kubomolewa,” alisema Heche kuelezea bomoabomoa hiyo itakatoyokana na utekelezaji wa sheria za nchi.
 
Akieleza zaidi, Heche alisema kuwa kwa kuanzia, NEMC imetangaza kuhakiki uhalali wa vibali vya wote waliojenga kwenye fukwe za bahari ili kubaini kama ni halali kweli na pia kujua ni ofisa au kiongozi gani wa serikali aliyevitoa, na kwa kutumia vigezo vipi.
 
Back
Top Bottom