Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bibi wa mwanafunzi wa darasa la tano anayesoma Shule ya Msingi Kilimanjaro wilayani Moshi, Costansia Lyimo amesema si mara ya kwanza kuwaadhibu wajukuu zake.
 
Akizungumza na Mwananchi jana baada ya juzi picha kusambaa zikionyesha mwanafunzi huyo akiwa amefungwa kwenye mti, Costantina alisema amekuwa akiwaadhibu wajukuu zake kwa namna hiyo ya kufungwa kamba na kutwishwa tofali kichwani huku akiwa amefungwa miguu na kunyanyua mikono juu ili liwe fundisho.
 
Alisema adhabu ambayo mwanafunzi huyo alipewa juzi ni kutokana na ukorofi wake kiasi ambacho wameshindwa kuvumilia na kwamba mara kwa mara akienda kuogolea huwa anakaa kuanzia asubuhi mpaka jioni.
 
Yaani huyu mtoto anaweza kuondoka nyumbani asubuhi hadi jioni ndio anaonekana, kwa kweli baada ya kaka yake kufunga shule na kurudi nyumbani nilimwomba anisaidie kumwadhibu maana ameshindikana,” alisema bibi huyo
 
Hata hivyo, mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Grace Mushi aliyekamatwa juzi jioni na kufikishwa katika kituo kidogo cha Polisi Majengo alisema mtoto huyo amekuwa akimsumbua kila mara kutokana na ukorofi wake.
 
Mwanafunzi huyo, alikiri kuwa huwa anapigwa na bibi yake huyo kila mara na kudai kuwa juzi ilikuwa si mara ya kwanza kupigwa ila kipigo kilizidi siku nyingine.
 
Kitendo cha kupigwa kwa mtoto huyo tulishindwa kuvumilia ilibidi twende kutoa taarifa katika kituo kidogo cha Polisi Longuo KCMC, ndipo baada ya muda kidogo askari kutoka kituo cha polisi Majengo walikuja kumchukua mtoto huyo pamoja na mama yake,” alisema shuhuda huyo.
 
2a3e5e6c17d239ebc017ccd956065361.jpg
 
Back
Top Bottom