Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkazi wa Kiangu, Edith Mboni ameiomba Serikali kujenga mitaro itakayopeleka maji baharini ili kuwaondolea adha hiyo.

Amesema mtaro uliopo ni mdogo hivyo kutokana na wingi wa maji unashindwa kuhimili.
 
Mkazi mwingine, Hassan Mbarali ameiomba Serikali kujenga miundombinu imara ili kuwaepusha na maafa ambayo yamekuwa yakijirudia mvua kubwa inaponyesha.

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Desemba 8,2017 ilitoa taarifa kwa umma ikieleza kuwapo vipindi vya mvua kubwa katika maeneo ya ukanda wa Pwani.

Maeneo hayo ni mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba.
 
Kwa sababu sisi ni binadamu sio malaika, kukosea ni miongoni mwa sifa zetu kuu. Hata hivyo, licha ya kwamba sote tunalifahamu suala hili lakini bado kuna nafasi ya kupewa adhabu pale tunapokosea.
 
Hapo sasa ndiyo zikaanzishwa jela, ili kwa wale ambao mahakama itajiridhisha kuwa wamekengeuka wawekwe humo kwa kipindi fulani wajifunze kutokurudia tena kuweka nyayo zao walipoziweka mwanzo.
 
Shuleni kukawepo na utaratibu wa kufeli, ili wale watakaojibu mitihani kwa majibu yanayowapendeza wao ilihali mitihani imetungwa na watu wengine, wanyooshwe.
 
Halafu kwenye ndoa nako kikatengenezwa kitu cha kuitwa talaka, ili kwamba mwanandoa mmoja anapokosea mwenzie awe na uwezo wa kumuadabisha—mwanamke adai talaka anapokosewa na mwanaume atoe anapoona inafaa.
 
Na kwa wale tunaoamini uwepo wa Mungu na shetani ibilisi pia tunaamini kutakuwa na moto baada ya kiama, moto maalumu kwa wote waliomkosea mwenye dunia yake, waliokwenda kinyume na maagizo yake – wataweka huko kuadhibiwa kwa kipindi fulani kulingana na makosa yao.
 
Hata hivyo, kuna makosa yanayoweza kuvumilika, ambayo unaweza kuyafanya na bado usipewe adhabu—ukasamehewa kabisa. Kosa kama kumdanganya anayekudai kuwa utamlipa jioni wakati unajua fika hali uliyonayo ulihitaji mkopo mwingine na sio kulipa deni.
 
Halafu kuna makosa ambayo mtu akifanya, hatakiwi kupewa tu adhabu, bali anastahili ashushiwe adhabu kubwa, nzito na ikiwezekana iwe ya kudumu. Kwa mfano, kosa kama la mwanaume kuingia kwenye uhusiano mpya katika mwezi Desemba.
 
Hili ni kosa la kijinga, nakukosea huku tunaita kwa kujitakia. Mwanaume mjanja, na mwenye akili zilizotulia unaanzaje kukubali kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mrembo kwenye msimu wa sikukuu namna hii? Ili Januari ikija uanze kuwasumbua watu kwa kuwapiga mizinga ya ovyo ovyo, sio?
 
Ukiingia kwenye mapenzi na mwanamke kwa kipindi hiki maana yake ni umeamua kuwa baba wa mtoto wa baba mwingine kwa sababu ni lazima utazama mfukoni kulipia gharama za kusuka manywele ya bei mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…