Waswidi wategua kitendawili
Wanasayansi wa Sweden wiki hii wamekuja na kile walichosema ni kubaini kile anachofanya nyuki ili asali isiwe na vimelea hatari vya magonjwa.
Katika ugunduzi wao wanasema unaweza ukasaidia fani ya sayansi ya afya juu ya namna ya kutengeneza dawa za kukabili maradhi mbalimbali yanayoenezwa na bakteria.
Wanasayansi hao wa Chuo Kikuu cha Lund nchini Sweden wamenukuliwa na Shirika la Utangazaji la BBC wakisema wamebaini kuwa katika tumbo la nyuki kuna kemikali ambazo zinatumika katika kuua aina yoyote ya bakteria hatari.
Tena wakasema kemikali hiyo huzalishwa na aina nyingine ya bakteria ambao hawa hukaa ndani ya tumbo la nyuki na kazi yake hiyo ni kutoa kemikali za kuua vimelea wowote hatari.
Kemikali inayotolewa na bakteria hai ni aina 13 za asidi zinazofanana na zile zinazopatikana kwenye maziwa.
Aina hizo 13 za asidi wamezielezea kuwa zimetengenezwa kwa kanuni maalumu ambayo inaua aina nyingi za bakteria wa maradhi.
Tunaweza kutumia kanuni ya ina hiyo kusaidia kutengeneza dawa ambayo haitamuathiri binadamu bali aina nyingi za bakteria hatari kwa afya ya binadamu,” anasema Dk Tobias Olofsson, mtaalamu wa Kitengo cha Tiba za Maradhi yaenezwayo na vimelea wa Chuo Kikuu cha Lund.
Kulingana na maelezo ya Dk Olofsson, bakteria hao ni sawa na kiwanda cha silaha ambacho kina wafanyakazi mahiri ambao wakiona tu aina ya adui, wanamtambua na mara moja wanaunda silaha ya itakayotumika kumuangamiza kulingana na umbile lake na maarifa yake katika kujihami.
Inaonekana kuwa mtindo huo kwa nyuki umedumu kwa mamilioni ya miaka na ndiyo maana nyuki hawadhuriki kiafya na asali wanayotengeneza ni salama pia kwa afya ya binadamu kwa sababu haina vimelea wa maradhi,” anasema mtaalamu huyo.
Kwa kawaida nyuki huvutwa na aina fulani ya umajimaji kwenye maua ijulikanayo kama nectar ambao huvutia wanyama ambao katika kuyavuna hujikuta wanausaidia kupevusha.
Wakati wa kutengeneza asali, nyuki hutoa vimeng’enyo kadhaa ambavyo katika hatua tofauti hufanikiwa kugeuza sukari iliyopo kwenye nectar kuwa sucrose, glukosi na fructose na baadaye ni gluconic ambayo ni asali.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.