Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Si Azory na watu hao wa Pwani pekee ambao wamekutana na mkasa huo, Aprili 6 wasanii wa muziki wa Hip Hop, Ibrahim Mussa maarufu ‘Roma Mkatoliki’ Monii Central Zone, Bin Laden na Imma, mfanyakazi wa mama mzazi wa mmiliki wa Studio za Tongwe Records iliyopo Masaki Dar es Salaam, J Murder walijikuta mikononi mwa watekaji.
 
Iliwachukua siku mbili wasanii hao kukaa kusikojulikana hadi April 8 walipopatikana lakini Roma ambaye hakueleza kinaga ubaga ni kina nani waliowateka akisema anaviachia vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi lakini mpaka sasa hakuna taarifa zozote za tukio hilo.
 
Akizungumzia matukio hayo, Dk Bisimba alisema mauaji na utekaji yaliyokuwa yakitokea enzi za utawala wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, kiongozi huyo alikuwa akijitokeza kuzungumzia na kukemea.
 
Mlinzi mkuu wa wananchi na mali zake ni Rais, matukio kama haya hatujaona akijitokeza kuyazungumzia na kuyakemea, yeye ndiye mwenye jukumu hili kwa hiyo ili mwaka 2018 yasijitokeze Rais asimame katika hili,” alisema.
 
Uvamizi wa Clouds

Haikuwahi kutokea tangu nchi ipate Uhuru pale Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na askari watano wenye silaha za moto, usiku wa saa nne, Machi 17 alipodaiwa kuvamia kituo cha Redio na Televisheni cha Clouds Media Group (CMG).
 
Ilidaiwa kuwa lengo la Makonda lilikuwa kuwashinikiza watangazaji wa kipindi cha ‘Shilawadu’ warushe video ya kumchafua Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
 
Tukio hilo lilimwingiza katika ugomvi mkubwa na wadau wa habari ambao walimtangaza kuwa adui wa tasnia ya habari pamoja na kumfungia kuripoti habari zake zuio ambalo lilidumu kwa zaidi ya miezi mitatu kabla ya kuondolewa pasi na kuomba radhi kama alivyopaswa.
 
Tukio hilo lilimfanya aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuunda kamati ya kuchunguza kitendo hicho lakini siku moja baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi, Rais Magufuli alitengua uteuzi wake, Machi 23 na nafasi yake kuchukuliwa na Dk Harrison Mwakyembe.
 
Ajali ya wanafunzi Lucky Vincent

Mei 6 ilikuwa siku ya simanzi na majonzi makubwa baada ya taarifa ya ajali mbaya ya basi lililokuwa limewabeba wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ya jijini Arusha waliokuwa wakienda kufanya mtihani wa ujirani mwema katika Shule ya Tumaini English Medium Junior.
 
Ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kutumbukia katika Mto Marera ulioko Mlima Rhotia, Karatu mkoani Arusha na kusababisha vifo 35 kati yake wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja huku wanafunzi watatu pekee; Doreen (13), Sadia (12) na Wilson (12), wakisalimika.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu aliratibu safari ya watoto hao walionusurika kwenda kupata matibabu zaidi katika Hospitali ya Mercy iliyopo Sioux City, Lowa nchini Marekeni kwa msaada wa Shirika la Siouxland Tanzania Educational Medical Ministries (STEMM).
 
Majeruhi hao waliondoka nchini Mei 15 kwa ndege maalumu ya Shirika la Samaritan’s Purse inayosimamiwa na mtoto wa mwinjilisti mkubwa wa Marekani, Franklin Graham ambayo pia iliwarejesha nchini Agosti 18.
 
Katika kuwaenzi waliofariki kwenye ajali hiyo, Bodi ya Wadhamini STEMM ilitangaza kuwasomesha watoto hao watatu hadi elimu ya Chuo Kikuu chochote duniani.
 
Kesi za vigogo

2017, pia umekuwa mwaka ulioshuhudia vyombo vya dola vikiwafikisha mahakamani vigogo mbalimbali kujibu tuhuma zinazowakabili na wengine mpaka sasa bado wapo korokoroni kutokana na kesi zao kutokuwa na dhamana.
 
Juni 19, sakata la ufisasi wa mabilioni ya akaunti ya Tegeta Escrow lilichukua sura mpya baada ya Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering & Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL),
 
James Rugemalira na mmiliki wa kampuni ya PAP, Habirnder Seth Singh walifikishwa mahakamani na Takukuru na kusomewa mashtaka kadhaa likiwamo la uhujumu uchumi. Kesi hiyo inaendelea na watuhumiwa wako rumande.
 
Viongozi wa michezo hawakuachwa salama na Takukuru baada ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wake, Celestine Mwesigwa na mhasibu Nsiande Mwanga, Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ pia walifikishwa na mahakamani na moja ya makosa wanayokabiliwa nayo ni la uhujumu uchumi.
 
Februari haikumwacha salama mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji alipofikishwa mahakamani akituhumiwa kutuma dawa za kulevya kisha akawa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi iliyomweka rumande kwa zaidi ya mwezi mmoja kisha kesi hiyo kufutwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
 
Vyombo kufungiwa

Mwaka huu unakwenda kumalizika huku ikishuhudiwa vyombo vya habari hususan magazeti yakifungiwa kwa vipindi tofauti. Magazeti yaliyofungiwa ndani ya mwaka huu ni MwanaHalisi, Mawio, Raia Tanzania na Tanzania Daima.
 
Dawa za kulevya

Februari, vita ya watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya ilichukua sura mpya baada ya Makonda kutangaza hadharani majina ya watu aliodai kuwa wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na biashara hiyo.
 
Back
Top Bottom