Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

But United rallied enough to win the match, even if they were hanging on at times by the end. There were positive performances too from the returning Luke Shaw and midfielder Scott McTominay, who was making only his second Premier League start. Marcus Rashford’s introduction on the three-quarter mark also helped to breathe fire into them on a bitter night.
 
97b3baa88693fc0662c3ffdef72e9de7.jpg
 
Wiki mbili zimebaki kuufunga mwaka 2017 na kuingia 2018. Kama ilivyokuwa kwa miaka mingine, 2017 umekuwa na milima na mabonde mengi, mambo kadha wa kadha yamejitokeza, ya simanzi na furaha.
 
Ni mwaka ulioshuhudia mapinduzi ya kimfumo hususan katika sekta ya madini baada ya Serikali kukunjua makucha kuhakikisha rasilimali hiyo ya Taifa inawanufaisha wananchi.
 
Baadhi ya matukio yaliyotikisa ni sakata la mchanga wa madini ya dhahabu (makinikia), kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ajali ya wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent, mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji, vigogo kufikishwa mahakamani, utekaji na shubiri iliyovipata vyombo vya habari.
 
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD), Dk Richard Mbunda anasema baadhi ya matukio yanaonyesha jinsi gani vyombo vya ulinzi na usalama vimeshindwa kutimiza wajibu wake.
 
Kuishi kwa woga, kuhofia kutekwa, atashambuliwa au atauawa, ilikuwa huko nyuma ili sasa imerudi. watu wanatekwa,” alisema Dk Mbunda.
 
Makinikia

Baada ya Rais John Magufuli kuunda tume mbili kuchunguza madai ya wizi na ufisadi unaodaiwa kufanywa na wawekezaji kwa zaidi ya miaka 19 iliyopita tangu walipoanza uzalishaji wa dhahabu, ilibainika kuwapo kwa kasoro kadhaa zilizolisababishia Taifa kukosa mapato.
 
Ripoti hizo ndizo zilizozaa mazungumzo kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold Corporation kuhusu kasoro zilizobainishwa na majadiliano yao yamekuwa yakielezwa na kiongozi wa timu ya Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi yanakwenda vyema na nchi itegemee kunufaika.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo Bisimba alizungumzia suala la makinikia akisema, “Ni suala zuri. Haki zetu za uchumi tulizopaswa kupata tunatakiwa tuzipate, lakini ninachojiuliza mwisho wa mazungumzo utakuwaje?”
 
Ripoti ya kamati ya kwanza iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma ilibaini kasoro za usimamizi na Rais Magufuli alimng’oa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika wadhifa huo na kuivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).
 
Pia, Rais Magufuli alimsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wake, Dominick Rwekaza na kuagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi dhidi yao ikiwamo watumishi wote wa TMAA na wakibainika hatua kali zichukuliwe.
 
Ripoti ya pili ya kamati maalumu chini ya Mwenyekiti Profesa Nehemiah Ossoro nayo ilibaini kuwa usafirishaji mchanga umelipotezea Taifa kati ya Sh132 trilioni na 380 tangu mwaka 1998.
 
Back
Top Bottom