Ni Kwanini Mlo Kamili Ni Muhimu Kwa Afya Ya Kinywa?
Kila mara unapokunywa ama kula kitu chochote cha sukari, meno yako hushambuliwa na tindikali (asidi) kwa muda kadiri ya saa moja. Hii ni kwa sababu sukari iliyopo kwenye hicho ulacho ama unywacho hutumiwa na bakteria walio katika utando mlaini ulio kwenye meno (Plaque) kutengeneza asidi.
Hivyo ni muhimu kuwa na vyakula vya sukari wakati wa milo rasmi kama vile mchana na usiku tu ili kupunguza muda ambao meno yako yatakua yanashambaliwa na tindikali itokanayo na kutumia vitu vya sukari.
Halikadhalika vyakula vyenye asili ya tindikali vinaathari pia, hii ni kwasababu tindikali huweza kuondoa tabaka la nje la meno(enamel) na kuacha tabaka la katikati (dentine) likiwa wazi. Hii huweza kuyafanya meno yaume pia.
Mlo ambao una vitamini, madini, matunda yalioiva vizuri na mboga za majani huweza kuzuia magonjwa ya fizi ugonjwa ambao huweza kupelekea meno kung’oka na harufu mbaya ya kinywa.
Ni Vyakula Gani Husababisha jino Kutoboka?
Kwa ujumla vitu vyote vya sukari husababisha meno kutoboka kutokana na kutumiwa na bakteria kutengeneza tindikali ambayo ndio hasa hutoboa meno
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.