Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vingi kati ya vyakula vya viwandani vina sukari na kadiri sukari hiyo ilivyoorodheshwa juu ndivyo ilivyo kwa wingi kwenye bidhaa husika. Hivyo ni vyema kusoma Maelezo yaliyo nje ya bidhaa mbalimbali unazo nunua madukani.
 
3fa06bba22054e1e6332fa9ee70193a7.jpg
 
Je Vyakula Na Vinywaji Husababisha Meno Kulika?
Ndio. Vyakula na vinywaji vyenye tindikali huweza kusababisha meno kulika kwani tindikali huweza kuondoa gamba la nje la meno (enamel). Ifuatayo hapa chini ni orodha ya pH ya baadhi ya vinywaji na vyakula. Chakula ama kinywaji chochote ambacho pH yake ni pungufu ya 5.5 huweza kusababisha meno kulika..
 
Je Ninaweza Kula Vitu Vyenye Sukari?
Kumbuka suala kubwa hapa si kiwango cha sukari una kula au kunywa, bali ni MARA NGAPI una kula ama kunywa. Vitu vya sukari vinaruhusiwa lakini ni muhimu kuvitumia wakati wa milo rasmi tu.
 
Je Ni Kinywaji Ninapaswa Kunywa?
Maji safi na salama na maziwa ni vitu vizuri kwa kunywa kwani ni rafiki wa meno yako. Ni vizuri pia kunywa juisi za matunda wakati wa milo rasmi na kama unakunywa kati ya mlo mmoja na mwingine, Jaribu kuchanganya na maji ili kupunguza kiasi cha sukari ambacho kinaweza kukutana na meno yako
 
Kula na kunywa vitu vya asidi (tindikali) kwa hakika hudhoofisha tabaka la enameli kwenye meno yako. Kupiga mswaki mara tu baada ya kula vitu hivi vya tindikali huweza kusababisha sehemu ndogo ndogo za tabaka la enameli kuondolewa na mswaki, hivyo inashauriwa kuwa mara ulapo ama unywapo vitu vya asidi kusubiri angalau saa moja ndipo upige mswaki.
 
Kwa hakika ni muhimu kupiga mswaki wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Hii ni kwa sababu utokaji wa mate hutumika kama namna ya kusafisha kinywa wakati wa usiku hupungua na hivyo kuacha kinywa katika hali hatarishi kwa kutoboka meno.
 
Kutoboka Kwa meno Na Fizi Zinazotoa Damu Ni Magonjwa Yaliyosambaa Sana
Takwimu zinaonesha kwamba magonjwa ya kinywa yanamuathiri kila mtu. Hakika hakuna nchi duniani ambayo haina matatizo yatokanayo na kutoboka kwa meno. Kutoboka kwa meno ni ugonjwa sugu kwa watoto matineja
 
Back
Top Bottom