Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tabia Njema kiafya Na Mitindo Ya Maisha Inayojengwa Utotoni Huweza Kudumu
Kuzuia ni mkakati muhimu katika kuhamasisha afya ya kinywa na meno miongoni mwa watoto. Nyingi ya tabia hatarishi na mitindo hatarishi ya maisha huweza kuchipukia katika umri wa shuleni, vivyo hivyo, tabia njema na mitindo ya maisha rafiki kwa afya ya kinywa huweza kujengwa na kudumu kama zitajengwa katika umri mdogo. Hivyo, kupiga mswaki kila siku kwa kutumia dawa ya meno yenye madini ya floridi ni tabia ambayo ni lazima ijengwe tangia utotoni.
 
Milo mizuri kwa afya ya kinywa pia ni lazima itiliwe mkazo tangia utotoni ili kuepuka kutoboka kwa meno. Kuanza kumpeleka mtoto kwa Daktari wa kinywa na meno tangia utotoni humfanya mtoto ajenge uhusiano wa kirafiki na watoa huduma hiyo ili kama kuna namna ya kuzuia magonjwa ya kinywa mapema kabla hayaja endelea sana na kuwa tatizo kubwa. Katika hili wazazi ni muhimu katika kutengeneza tabia chanya na rafiki kwa afya ya kinywa na meno.
 
Kuna hatari ya wewe mwenyewe kuchukiwa na muhusika kwakua ataona umemuaibisha na kujisikia vibaya ama hata asiweze kuzungumza na wewe tena! Japokuwa, ina faida kukumbuka kuwa harufu mbaya ya kinywa husababishwa na matatizo mbalimbali. Hivyo mara mtu ajuapo kwamba ana tatizo hili, huweza kuchukua hatua kadhaa katika kutafuta msaada. Hivyo unaweza kuongea hata na ndugu ama jamaa wa karibu kuhusu tatizo la mwenzio kama wewe mwenyewe unashindwa kuongea nae ili tu apate msaada unaostahili
 
Meno ya kwanza ya utu uzima huanza kuota kinywani mtoto wako anapofikisha umri wa miaka 6, wakati huohuo meno ya utotoni huanza kung’oka, kwa lugha nyepesi meno ya kiutu uzima huja kuchukua sehemu ya meno ya utotoni. Ni kawaida kwamba meno ya chini ya utotoni ndio huanza kung’oka kisha kufuatiwa na meno ya juu kipindi kifupi baadae.
 
Mtoto anapofikisha umri wa miaka 13 huwa na meno yote ya ukubwani isipokuwa magego ya mwisho (Third molars/Wisdom teeth) ambayo huota na kujitokeza kinywani wakati wowote kati ya miaka 18 na 25. Zingatia kwamba watoto hutofautiana na hata uotaji wa meno huweza kutofautiana.
 
Back
Top Bottom