Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je Ninapaswa Kutumia Dawa Ya Meno Yenye Madini Ya Floridi?
Ndio unapaswa kutumia dawa ya meno yenye madini ya floridi hata kwa mtoto mdogo kwani dawa hii itumikapo kwa ukamilifu huweza kutoa ulinzi kamili kwa meno yako dhidi ya magonjwa ya kutoboka meno.
 
Je Ni Mswaki Aina Gani Unafaa Kwa Watoto?
Kuna miswaki ya aina mbalimbali kwa ajili ya watoto na yote huweza kusafisha meno vizuri. Ni vizuri ukaenda dukani na mtoto ili aweze kujigulia mswaki autakao, hii itamtia moyo kupiga mswaki. Kitu muhimu ni kuwa Na mswaki wenye kichwa kidogo na visafishio laini kulingana na umri wa mtoto wako
 
Je Ni Nini Kinaweza Kusababisha Mtoto Wangu Kuumwa Na Jino?
Maumivu yatokanayo na jino ni makali na yanatisha hasa kwa watoto, sababu kubwa huwa ni kutoboka, hali ambayo husababishwa na ulaji wa vyakula vyenye sukari kwa wingi kwenye milo yetu na pia kutokuwa makini na upigaji wa mswaki
 
Hali kadhalika kuota meno wakati mwingine huweza kuambatana na maumivu hali ambayo huanza mtoto anapofikisha miezi 6 na huweza kuendelea hata wakati meno ya kiutu uzima yanapoanza kuota. Kama kutakua na umuhimu wa kumpa mtoto dawa ya kutuliza maumivu, mpatie zile ambazo hazina sukari. Kama maumivu yataendelea ni vizuri kumuona daktari wa kinywa na meno mapema.
 
Kama unataka kumpa mtoto wako chakula kati ya mlo mmoja na mwingine ni vizuri kumpa vitu visivyo vya sukari kama vile maji ama maziwa. Na muhimu zaidi ni kwamba kupiga mswaki kwa umakini wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala husaidia sana kuzuia kutoboka kwa meno.
 
Back
Top Bottom