Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

na hakika watoto na matineja wengi hupata maumivu yatokanayo na meno yaliyotoboka, huku wengi wao wakiwa na meno yaliyotoboka bila kutibiwa kwa muda. Halikadhalika fizi zinazotoa damu ni ugonjwa unaoathiri karibu kila mtu
 
Those beautiful dimples and sexy eyes!
25022912_166012144152339_1357734751057739776_n.jpg
Mmhhh jaman hawa wapo wapi
 
na hakika watoto na matineja wengi hupata maumivu yatokanayo na meno yaliyotoboka, huku wengi wao wakiwa na meno yaliyotoboka bila kutibiwa kwa muda. Halikadhalika fizi zinazotoa damu ni ugonjwa unaoathiri karibu kila mtu
 
Watoto Wengi Na Wazazi Wao Hawana Taarifa Na Elimu Ya Sahihi Na Ya Kutosha Kuhusu Afya Ya Kinywa
Katika nchi nyingi mbalimbali, watoto na Matineja wengi wana uelewa mdogo sababu ya magonjwa ya kinywa na namna ya kuyazuia. Halikadhalika hata kina mama ambao ni walezi wakubwa na watu wa karibu ufahamu wao ni mdogo pia
 
kana kwamba hiyo haitoshi na walimu ambao labda wangeweza kuwafundisha kuhusu afya ya kinywa wakiwa mashuleni nao pia ufahamu wao ni mdogo hata kama ni wa juu ukilinganisha na wazazi ama walezi wa watoto hao. Kuna ushahidi kwamba imani potofu zina mchanga katika ufahamu wa sababu za magonjwa ya kutoboka meno na fizi zinazotoa damu,
 
hii hupelekea watu wengine kuamini kwamba magonjwa haya ni ya kurithi. Ni kiasi kidogo tu cha watoto, wazazi na walimu ambao wana ufahamu wa kutosha juu ya madhara ya vyakula na vinywaji vya sukari kwenye afya ya kinywa. Zaidi sana, wakati wazazi wengi wanafahamu juu ya umuhimu wa kupiga mswaki kwa ujumla
 
lakini baadhi hawajui namna ya kuzuia kutoboka kwa meno na fizi zinazotoa damu, Halikadhalika hawafamu juu ya kazi ya madini ya floridi katika kuzuia kutoboka kwa meno. Pia Tafiti zinaonesha kua ni chini ya asilimia 50 ya akina mama ndio ambao wamewahi kupata ushauri kutoka kwa madaktari wa kinywa kwa meno
 
Watoto Wengi Huiga Tabia na Matendo Ambazo Si Rafiki Kwa Afya Ya Kinywa
As part of oral hygiene routine self-care, individuals should clean their teeth and gums every day with fluoridated toothpaste. However, in many countries the proportion of children who brush their teeth every day is still unsatisfactory. This means that schools may be the only place where children can carry out oral hygiene practices and being followed up successfully.
 
Magonjwa Ya Kinywa Yanapogundulika Mapema Yanazuilika Kabisa
Ukweli ni kwamba magonjwa ya kinywa yaliyojijenga kwa muda mrefu hayarekebishiki. Kwa mfano unapokuwa na tundu kwenye jino lako hasa katika jino la utu uzima, tundu hilo huendelea kuwepo katika maisha yako yote. Na hata kama jino lako litazibwa, kiraka hicho kitabakia kinywani mwako maisha yako yote. Hata hivyo,
 
ni lazima isisitizwe kwamba panapofanyika hatua stahiki, magonjwa ya kinywa kama vile kutoboka kwa meno ama fizi zinazotoa damu hupona, huzuilika na kuepukika. Kinyume chake ni kwamba, magonjwa yaliyojijenga kwa muda mrefu huwa na madhara makubwa na ni vigumu kuyatibu. Ni wazi kuwa kuzuia ni bora kuliko kutibu.
 
Madhara Na Gharama ya magonjwa Ya Kinywa Ni Makubwa
Kwa watoto magonjwa ya kinywa yasipotibiwa hupelekea maumivu, kushindwa kula vizuri, kushindwa kujisomea na hata kutokwenda shule. Kuchelewa kwa matibabu sio tu hutoa nafasi kwa ugonjwa kujijenga zaidi na kuwa sugu, bali pia hata gharama za matibabu huongezeka.
 
Matokeo ya kushindwa kumudu gharama za matibabu hali ambayo husababisha mtoto kung’olewa jino ama meno kama mbadala wa kushindwa kumudu gharama kubwa za matibabu. Halikadhalika uzoefu mbaya ambao mtoto anaupata utotoni hupelekea kuchukia hata watoa hudumu ya afya ya kinywa hivyo kuendelea kuwa na afya mbovu ya kinywa yeye mwenyewe.
 
Afya Mbaya Ya Kinywa Huathiri Kusoma Na Afya Ya Jumla Ya Mwili
Kupata maumivu, jipu, kushindwa kula na kutafuna vizuri, kujisikia vibaya kutokana na meno kuoza na kubadilika rangi kunaweza kumfanya mtoto akajitenga na wenzake kwenye michezo na hata kujisomea kwa bidii. Hali kama hii inapoachwa hata kama ni kwa muda mfupi huwa na madhara kwa afya ya mtoto.
 
Afya Mbaya Ya Kinywa Huathiri Kusoma Na Afya Ya Jumla Ya Mwili
Kupata maumivu, jipu, kushindwa kula na kutafuna vizuri, kujisikia vibaya kutokana na meno kuoza na kubadilika rangi kunaweza kumfanya mtoto akajitenga na wenzake kwenye michezo na hata kujisomea kwa bidii. Hali kama hii inapoachwa hata kama ni kwa muda mfupi huwa na madhara kwa afya ya mtoto.
 
makuzi ya mtoto husika pia huathirika ikiwemo hata ukuaji wa meno na kinywa kwa ujumla, hali ambayo huweza kurahisisha kupatikana na magonjwa ya kinywa na meno kwa mtoto husika ukiacha magonjwa mengine ya mwili.
 
Ni rahisi Sana Kuzuia Magonjwa Ya Kinywa Kwa Watoto Kupitia Shule
Kufundishwa namna ya kutunza kinywa, kufundishwa namna ya kujua milo mizuri, kupata matibabu ya kinywa wakiwa shuleni ni namna bora na rahisi ya kuwawezesha watoto kuzuia magonjwa ya kinywa na meno na madhara yake, hivyo kuwafanya kuwa na afya njema ya kinywa na meno
 
Back
Top Bottom