hata hivyo amesema kujua aina nyingi zamapishi kutaepusha tatizo linalozikumba baadhi ya familia kwa watoto kutojua kupika na pale wanapoozeshwa mapema hulazimka kuachwa nakurejehswa nyumbani mapema kwa kosa kama hilo.
Akitoa maoni yake amewataka wakuu wa familia wasiwe wavivu katika kuwafundisha watoto wao kupika , kwani watoto ndio ngao ya taifa pamoja wazazi wa baadae.
alisema kuna baadhi ya familia ambazo zinajipata huweka wafanyakazi ndani na kazi zote humaliza mfanyakazi na kumuacha mwanawe kutulia juu ya kioo cha televisheni.
Alisema hilo ni kosa kwa wazazi ambao wanafanya hivyo kwani mwisho wa siku kupata aibu ndani ya familia ile kuonekana haina madili mazuri ndani ya nyumba hiyo.
Hasara za achari.
Ingawa achari ni kitoweo lakini, ina hasara kwa binaadamu kwani haikatazwi kutumia mpaka kusababisha michubuko ya tumbo na kukataa mafuta ndani ya mwili na kusababisha kawa vidonda vvya tumbo ikiwa na `ndio chanzo cha maradhi ya tumbo ni na kukosa uzazi na mengineo.
Makala hii ilikutana na Daktari wa magonjwa ya tumbo Dr Ibrahim Mohammedi Saleh alisema “mara kwa mara wagonjwa wa aina hii huwa ni wakaidi hata ukawafahamisha athari za utumiaji wa vitu vikali,huhisi kama unawaonea’’
kitaalamu ukila vitu vikali katika tumbo kuna kitu kinatengenezwa kinaitwa citric juice,hivyo hii huharibu kuta za tumbo na kuzalisha gesi kwa wingi ambapo humfanya mlaji apate maumivu makali na kumpelekea kupata maradhi mbali mbali vikiwemo vido
UFUGAJI WA SAMAKI JINSI UNAVYOMSAIDIA MTU MWENYE KIPATO CHA CHINI
Suala la ufugaji wa samaki si suala muhimu kwa kukuza maisha na kipato chamtu ua watu
Kama inavyoonekana kwa kikundi cha Kupata si kukosa kilichopo katika kijiji cha Pujini Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Pemba walivyofaidika kwa ufugaji wa samaki.
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wenzake katibu wa kikundi hicho Bw Yahya Muhamed Maalim alisema kunafaida nyingi wanazozipata katika ufugaji huo wa samaki kwa kuimarisha maisha yao kwani kikundi hicho walikuwa hapo mwanzo ni watu wa vijiweni tu lakini sasa muda mwingi wanautumia kwa kuzalisha .
Vile vilie alisema katibu huyo kuwa kuwa ufugaji wa samaki umewapatiya kipato kizuri kwa muda mfupi wameweza kuona mabadilikona sioa kama mwanzo walivyokuwa wakikaa katika vijiwe.
Hata hivyo Bw Maalim alisema zipo changamoto nyingi katika ufugaji wa samaki ambazo ni kama vile kukosa soko zuri la kuuzia samaki,kipindi cha kuvua samaki hubidi kuuza bei ya chini hufanya kufeli kwa mipango yao.
Pia ukosefu wa elimu ya kitaalamu ya ufugaji wa samaki ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili kwani mpaka sasa bado hawajapata elimu bora kwa ushirika huokwani wakati wanapotaka kuendeleza ufugaji wa samaki wanatumia elimu ya kusimuliwa kitu ambacho kinaweza kuwarudisha nyuma katika ushirika wao na ado wanaona wanafanya kitu kisicho na uhakika katika misha yao .
Kwaupande wake mshika fedha wa kikundi hicho Bi Halima Khatibu Omar alisema ufugaji wa samaki unawapatia kipato kikubwa kwani unawasaidia kupata rizki ndogo ndogo kutokana na umuhimu wa kimaisha ,na endapo Baba amekosa basi unaweza kutoa hakiba ulioipata ili kusaidia maisha.