Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umuhimu wa ikolojia ya Serengeti

Robert Fyumagwa ambaye ni mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri), kituo cha Serengeti anasema nyumbu wamepungua kwa asilimia 40 kutokana na kasi ya ujangili inayoendelea ndani ya ikolojia hiyo muhimu kiutalii duniani.
 
Mtafiti huyo anasema ikolojia hiyo yenye mita za mraba 30,000 ikiundwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mapori ya akiba ya Ikorongo, Grumeti, Maswa, Kijereshi, Pori Tengefu la Loliondo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi za Jamii za Makao, Ikona na Masai Mara nchini Kenya, ina maajabu ambayo hayapo sehemu yoyote duniani.
 
Kipindi hatari

Kwa mujibu wa mmoja wa wahifadhi, ujangili wa waya huongezeka kuanzia Julai kila mwaka maeneo ya Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kipindi ambacho makundi makubwa ya nyumbu na pundamilia yanapokuwa yanaingia kutoka Maasai Mara Kenya na wakati wa kurudi.
 
Maeneo ya Ndabaka ujangili unaofanyika ni wa kutumia pikipiki kuwafukuza wanyama kwa kuwa ni peupe, lakini huku Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wanatumia mitego, kipindi wanapovuka nyumbu wengi huuawa na majangili,”anasema.
 
Maeneo ya Ndabaka ujangili unaofanyika ni wa kutumia pikipiki kuwafukuza wanyama kwa kuwa ni peupe, lakini huku Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wanatumia mitego, kipindi wanapovuka nyumbu wengi huuawa na majangili,”anasema.
 
Anasema majangili hutandaza nyaya nyingi katika eneo ambalo wanapita ama eneo lenye maji. Kila jangili anaweka alama kwenye mtego wake ili kuepuka ugomvi baada ya kunasa, wanachofanya ni kuwafukuza ili wapite eneo hilo na hapo hunaswa wengi.
 
Wanatega karibu na makorongo na wakati mwingine huweka magogo karibu na eneo wanapokunywa maji; wanapoingia hapo huwa rahisi kuwanasa, kazi hiyo hufanywa jioni kisha huacha mitego na kurudi kwenye kambi zao ambako hukaa na alfajiri huwahi kuangalia mavuno ya kazi yao,” anabainisha mhifadhi huyo.
 
Anakiri kuwa kwa wakati mmoja huweza kunasa wanyama zaidi ya 100 na huwasomba kwa kutumia baiskeli na vichwa hadi kwenye kambi ambako hukausha nyama maarufu kama (Vimoro) ambazo huzisafirisha nje ya hifadhi na wateja kununua kwa ajili ya kuuza maeneo mbalimbali.
 
Ukubwa wa tatizo

Licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (Tawa), Grumeti Reserves na wengineo kukamata majangili na waya, bado kasi ya ongezeko ni kubwa na kuhatarisha uendelevu wa uhifadhi wa wanyamapori.
 
Uchunguzi wa Mwananchi ulibaini kuwa zaidi ya mitego ya waya 130,729 ilikamatwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kipindi cha miezi 23 kutoka Juni 2015 hadi Juni 2017. Aidha, kwa kipindi cha miezi sita mwaka 2015, mitego 26,923 ilikamatwa.
 
Kwa mwezi Julai tulitegua mitego 8383, Agosti 9581 na Septemba 7332, kwa ujumla kuanzia Julai hadi Novemba ujangili huwa juu kwa kuwa wanyama kama nyumbu na pundamilia wanakuwa wanaingia, hasa kwa maeneo ya Wilaya ya Tarime na Serengeti upande wa Kaskazini mwa hifadhi,” anasema.
 
Back
Top Bottom