Wateja zaidi ya 30 waliolipa ankara za maji na fedha zao kudaiwa kutafunwa akiwamo mfanyabiashara wa nyumba za kulala wageni aliyelipa Sh700,000, Msafiri Lugega aliyesema uaminifu ni jambo kubwa na muhimu maishani.
Hili limebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa Vodacom, Ian Ferrao aliyezungumza na gazeti hili baada ya kuulizwa kuhusu usalama wa fedha za wateja wa M-Pesa ambao kwa sababu moja au nyingine hawatumii akaunti zao kwa muda mrefu.
“Akaunti huendelea kuwa hai kwa siku 270 baada ya hapo salio lililopo huhamishiwa Benki Kuu na akaunti kufungwa kwa mujibu wa sheria. Endapo mteja atajitokeza, salio lake hurudishwa,” alisema Ferrao.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa wa Benki Buu (BoT), Benerd Dadi alithibitisha kuwapo kwa sheria inayoweka sharti hilo kwa kampuni za simu zinazotoa huduma za fedha.
Kampuni za simu hazitunzi fedha. Fedha zote za wateja zinahifadhiwa kwenye akaunti ya benki inayoitwa Trust. Mteja ambaye hajatumia simu yake kwa muda mrefu, salio lake huhamishiwa Benki Kuu kwa mujibu wa (Sheria ya Mali Iliyosahaulika) Unclaimed Property Act,” alisema Dadi.
Endapo mteja husika hatajitokeza kwa muda muafaka, fedha hizo huhamishiwa serikalini kama inavyoagizwa na utaratibu uliopo. Kwa upande wa mifumo ya malipo, hususan miamala ya fedha kwa njia ya simu, kifungu cha 31 cha Kanuni za Fedha za Miamala 2015 husimamia utaratibu huu.
Kwa mujibu wa kanuni hiyo, kigezo kikubwa kinachozingatiwa kuifanya akaunti ionekane imetelekezwa ni ukomo wa miaka mitano pasipo mwenye akaunti kujitokeza. Baada ya muda huo kupita bila mwenye akaunti kujitokeza, Benki Kuu huziwasilisha fedha husika serikalini kupitia kwa Msajili wa Hazina baada ya kuzipokea kutoka kwa watoa huduma.
Alifafanua kuwa endapo mteja wa akaunti hiyo atapatikana au mrithi wake akajitokeza, akikamilisha taratibu za mirathi, basi kampuni husika ya simu humsaidia kupata fedha zake.
Asipojitokeza kwa miaka 15 Serikali huzitumia,” alifafanua.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Benki na Taasisi za Fedha wa BoT, Kennedy Nyoni alisema utaratibu huo pia hutumika kwenye akaunti za benki za biashara ambako mteja asiyeitumia kwa miaka 15 mfululizo, salio lake lililopo huhamishiwa BoT.
Kama mteja wa fedha au mali iliyohifadhiwa benki asipoonekana kwa muda huo, huhesabiwa kama (mali iliyotelekezwa) abandoned property. Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha inaagiza hivyo,” alisema Nyoni.
Baada ya miaka 15 ya fedha hizo kutunzwa BoT, huwasilishwa serikalini ambako hupangiwa matumizi kwa mujibu wa sheria. Jitihada za kutafuta taarifa za matumizi ya fedha hizo hazikuzaa matunda.
Msajili wa Hazina, Dk Oswald Mashindano alisema tangu aanze kuiongoza ofisi hiyo hajawahi kupokea fedha kutoka kwenye akaunti hiyo na akashauri taarifa hizo zitafutwe ofisi ya katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.