1. POTOFU: Kupiga mswaki mara nyingi na kwa nguvu huzuia kuoza kwa meno
UKWELI: Si mara ngapi unapiga mswaki na nguvu gani inatumika, suala ni unapigaje mswaki. Kupiga mswaki mara nyingi na kwa maguvu kunaweza kupeleke kukwangua sehemu ngumu ya nje ya jino, kulifanya laini na hatimaye kuuma au hata kuvunjika. Kupiga mswaki mara mbili, taratibu na kwa njia sahii ndicho kinachosaidia meno kuwa na afya