Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Winnie, 81, ni mwanamama aliyejipatia sifa kutokana na kushiriki kikamilifu harakati za kupambana na utawala wa ubaguzi na aliwahi kuteswa na mamlaka za utawala wa weupe wachache, lakini hakutetereka na akaja kuwa waziri katika serikali ya kidemokrasia mwaka 1994.
 
Familia ya Mandela inapenda kuutaarifu umma kwamba Winnie Madikizela-Mandela Jumapili alilazwa katika Hospitali ya Milpark," ilisema sehemu ya taarifa hiyo kuhusu mama huyo aliyeolewa na Nelson mwaka 1956 lakini wakatalikiana mwaka 1996.
 
Mwanakwaya wa kwaya ya Mtakatifu Secilia, Kigango cha Muze Parokia ya Zimba, Jimbo Katoliki Sumbawanga, Flora Nandi (25) ameanguka na kufariki dunia muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya shukrani akiwa kanisani.
 
Akizungumzia tukio hilo, mwalimu wa kanisa aliyekuwa akiongoza ibada hiyo, Katekista Philipo Lupadasi alisema wanakwaya wakiwa wanaimba na marehemu akiwa ametoka kutoa sadaka ya shukrani alirejea katika sehemu yake kwenye kwaya na kuendelea kuimba lakini ghafla alianguka chini hali iliyozua mshtuko na kusababisha ibada kusimama kwa muda.
 
Alisema wanakwaya wenzake walimnyanyua na kumtoa nje ya kanisa ili apate hewa wakiamini kuwa amepoteza fahamu. Katekista huyo alisema baada ya kumpepea kwa muda, waliona hapati fahamu hali iliyowalazimu kumpeleka Zahanati ya Kijiji cha Muze kwa ajili ya matibabu.
 
Baada ya kupewa taarifa za kifo hicho, wanakwaya hao waliangua kilio na hawakuweza kurudi tena kanisani kuimba katika ibada ya pili na badala yake waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka nyumbani kwake kwa taratibu za mazishi.
 
Mwalimu wa kwaya hiyo, Aloyce Mwandanje alisema kuwa kifo cha mwanakwaya mwenzao ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi mitano, kimewaachia majonzi makubwa lakini hawana la kufanya kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu.

Alisema mwili wa marehemu Nandi ulizikwa Jumatatu katika makaburi ya Kijiji cha Muze.
 
Jaji mstaafu Robert Kisanga amefariki dunia.

Rais wa Chama cha Majaji Wastaafu, Thomas Mihayo akizungumza na MCL Digital leo Jumatano Januari 24,2018 amesema Jaji Kisanga alifariki dunia jana jioni.

Jaji Mihayo amesema Kisanga alifariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam.

Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Mbali ya shughuli za Mahakama, Jaji Kisanga alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini.
 
Saratani ya utumbo ni chanzo cha kifo cha Jaji mstaafu Robert Kisanga, imeelezwa.

Msemaji wa familia, Dk Onesmo Kisanga amesema Jaji Kisanga alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa miaka minne.
 
Akizungumza na MCL Digital leo Jumatano Januari 24,2018 nyumbani kwa marehemu Oysterbay, Mtaa wa Bongoyo, Dk Kisanga amesema jaji huyo aliwahi kwenda nchini India kwa matibabu mara mbili.

Amesema Jaji Kisanga alipatiwa dawa ambazo alikuwa akiendelea kuzitumia hadi alipofariki dunia jana jioni Jumanne Januari 23,2018.
 
Kwa muda mrefu alikuwa anaumwa lakini wiki mbili zilizopita hali yake ilikuwa mbaya zaidi ndipo daktari wake alipoelekeza akalazwe hospitalini kwa uangalizi zaidi," amesema Dk Kisanga.

Amesema juzi Jumatatu Januari 22,2018 hali yake ilibadilika akawekwa chumba cha wagonjwa mahututi na jana saa 12:30 jioni alifariki dunia.
 
Kuhusu utaratibu wa mazishi, Dk Kisanga amesema, "Bado hatujapanga ndiyo kwanza naenda Mahakama Kuu. Jioni tutakuwa na kikao ndipo itafahamika mazishi yatakuwa lini ila ni kati ya Jumamosi na Jumatatu."
 
Wakazi wa Karatu na baadhi ya wabunge wamejitokeza kuaga mwili wa mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Moshi Darabe (57).

Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii waliopo wilayani Karatu wameshiriki shughuli hiyo leo Jumatano Januari 24,2018 wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Kemilembe Luota.
 
Shughuli ya kuaga mwili imefanyika katika viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu na mazishi yatafanyika katika Kata ya Baray.

Wabunge kutoka CCM waliokuwepo ni Nape Nnauye wa Mtama, Mary Chatanda (Korogwe) na Joseph Musukuma (Geita Vijijini).
 
Kutoka Chadema wabunge waliokuwepo ni Willy Qambalo wa Karatu, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki); Lucy Owenya na Grace Kiwelu (Viti Maalumu).

Darabe aliyekuwa diwani wa Baray alifariki dunia Jumapili Januari 21,2018.

Alikuwa mwenyekiti wa Chadema wilayani Karatu tangu mwaka 2003 na alishika wadhifa wa udiwani kuanzia mwaka 2000.
 
Back
Top Bottom