1. Kila wakati, pambana na mambo magumu, wakati mambo hayo bado ni rahisi. Pambana na changamoto zako, wakati changamoto hizo bado ni kidogo. Pambana na kuitunza afya yako, wakati bado umzima. Pambana na umaskini, wakati bado ukijana mwenye nguvu.
Kila changamoto unayokutana nayo kwenye maisha, unaweza kuishinda ikiwa utakabiliana nayo mapema. Acha kusubiri mambo yameharibika ndio uanze kukomaa na changamoto yako. Acha kusubiri nyumba imeungua ndio utafute maji ya kuzimia moto.