Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20180126-WA0039.jpg
 
Basi nadhani nisizungumze sana niende moja kwa moja katika somo ambalo nimelikusudia, najua fika wapo baadhi ya watu kwao mikopo ni rafiki , wapo pia baadhi ya watu ambao mikopo kwao imekuwa ni adui mkubwa sana, hii ni kutokana na matokeo ya mikopo hiyo.
 
Pia mikopo hiyo ipo ya aina mbalimbali kwa mfano;
(a) mikopo midogo midogo- hii ni mikopo ambayo hutolewa kwa jamii, kwa ajili ya kuendeleza biashara ndogo ndogo. Lengo la mkopo huu husaidia kuongeza mtaji katika biashara ndogo ndogo ili kuwa biashara kubwa.
 
Hizo ni baadhi za aina ya mikopo ambayo hutolewa kwa wanajamii lakini zipo aina nyingi za mikopo. Lakini katika makala haya naomba nijikite zaidi katika siri ambazo zimejificha katika mikopo ya kibiashara maana huku ndiko ambako watu wengi hasa wafanyabiashara wengi waichukue mikopo hiyo, na watu wachache ndio ambao wana urafiki na mikopo hiyo ya kibiashara. Je nini kinachosababisha hali hiyo?
 
Zifuatazo ndiyo siri ya mkopo iliyojificha.

1. Usichukue mkopo kama biashara yako haifanyi vizuri.
Watu wengi hususani hawa wanaoichukia mikopo ya kibiashara, wengi wao huchukua mikopo hasa pale ambapo biashara inapokwenda vibaya, lakini kufanya hivi ni kosa kwa sababu wateja wengi huwa wamepotea hivyo ukichukua mkopo itakuwa ni kazi bure kwani wateja watakuwa wachache hivyo suala la marejesho kwako litakuwa ni suala gumu sana, ila ili kuufurahia mkopo wa kibiashara hakikisha unachukua mkopo wakati biashara inakwenda vizuri, kwani kufanya hivi wateja watakuwa wengi pia itakuwa ni rahisi kwako kurejesha marejesho ya mkopo huo.
 
2. Chukua mkopo kwa lengo ulilokusudia.
Mara zote watu wengi huuchukia mkopo wa kibiashara kwa sababu malengo ya kuchukua mkopo huo hufanya kazi ambazo huzikustaili, kwa mfano utakuta mtu amechukua mkopo kwa kuendeshea biashara lakini cha ajabu pale mtu huyo apewapo mkopo huo utashangaa anafanyia kitu kingine kama vile ulipaji karo, kodi ya nyumba n.k. lakini kufanya hivi ukumbuke ya kwamba ni kupoteza maono sahihi ya kibiashara na mwisho wa siku kupelekea biashara kufa.
 
Back
Top Bottom