Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni jambo la kawaida kuachwa na usafiri kama vile basi, boti, treni au ndege licha ya kufanya maandalizi ya kutosha. Baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia mtu mpaka kuachwa na usafiri ni kama vile foleni barabarani, ajali au usafiri kupata matatizo na kukosea muda wa kuwasili.
 
f2736f5b2f22e1238c918103a007a277.jpg
Duh
 
kuwasili.Hali ya kuachwa na usafiri ni ngumu sana kama haijawahi kukutokea kabla na hauna mbinu mbadala ya kukuwezesha kusafiri kama ulivyokukusudia. Zipo hatua kadhaa za kufuata pindi uchelewapo ndege ambazo Jumia Travel ingependa uzifahamu na kuzizingatia pindi utakapokumbwa na changamoto kama hii.
 
Wasiliana na shirika la ndege unalosafiri mara moja. Kitu cha kwanza kabisa baada ya kugundua kwamba utachelewa au umechelewa ndege ambayo ulitakiwa kusafiri nayo ni kuwasiliana na shirika husika. Mara nyingi mawasiliano huwemo kwenye tiketi au tovuti ya shirika. Kwa kufanya hivyo utajua ni msaada gani wanaweza kukupatia kulingana na hali uliyopo.
 
Kuwa makini na sheria na masharti ya tiketi uliyokata. Kila shirika la ndege linakuwa na taratibu za uendeshaji wa safari zake. Zipo ambazo zinawasafirisha na ndege nyingine wateja wao waliochelewa, zingine siku inayofuata kama hamna kwa siku hiyo na zingine kutoza malipo ya ziada kwa kuchelewa ndege. Kwa hiyo kabla ya kukata tiketi ulizia taarifa hizo au soma kwenye tiketi yako kama zipo.
 
Usipohamaki utaweza kupata suluhu ya tatizo haraka sana kama vile kuulizia cha kufanya, kuahirisha au kutafuta uwanja wa ndege ulio karibu ili usafiri na kuwahi shughuli zako kama ulivyopanga. Kwani kama kuchelewa umekwisha chelewa hakuna cha kufanya kutokana na hali hiyo.
 
Ulizia kwa wafanyakazi wa kampuni husika ya ndege machaguo uliyonayo. Kama umeshindwa kupata mawasiliano au haujui taratibu za shirika la ndege ulilokatia tiketi ya kusafiri basi ni vema ukauliza. Mashirika mengi yanakuwa na ofisi k
 
Lipia gharama za ziada baada ya kukosa ndege kama ulishafika tayari. Kama unaona kwamba utachelewa shughuli zako huko uendako basi huna budi kuongeza pesa kidogo ili uweze kusafiri na ndege inayofuata
 
Hii itakuwa nafuu zaidi kuliko kukata tiketi upya au kuahirisha safari. Kwa hiyo ni vema pia kuwa na fedha au chanzo za ziada pindi unapokuwa unasafiri kwani chochote kinaweza kutokea.
 
Tazama kama kuna ndege zingine zinazoelekea mahali uendapo. Kwa kawaida kwenye viwanja vya ndege vingi kunakuwa na ubao unaoonyesha ndege za mashirika tofauti zinazokwenda sehemu mbalimbali kwa siku hiyo. Hivyo inaweza kuwa fursa kwako kwa kufanya maamuzi ya kukata tiketi ili kuwahi shughuli zako.
 
Back
Top Bottom