Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

bf5fcf74e25b39534de806e57417d1a4.jpg
 
Kila siku teknolojia inakua kwa kiwango kikubwa na imekuwa na manufaa mengi kwa wanadamu. Ukuaji wa teknolojia umepelekea urahisi katika kufanya mambo magumu kuwa mepesi. Hili limechangia katika kupunguza muda na nguvu iliyokuwa ikitumika hapo awali katika kufanya jambo hilo hilo kwa kutumia nguvu kubwa.
 
Kwa upande wa magari, teknolojia imetuwezesha watu wengi kupata urahisi katika uendeshaji wake kwani magari ya saa ‘automatic’ yamerahisishwa sana tofauti na magari ya manual ambayo yalikuwa yakiwatatiza watu wengi, hasa wanawake.
 
Kuna tofauti kubwa sana ya kiutendaji kati ya magari haya ya automatic na yale ya manual. Magari haya ya automatic ni rahisi sana kuyaendesha kwa kuwa sehemu kubwa ya mfumo wa utendaji wake ni wa kisasa kabisa na kujiendesha wenyewe. Ila kuna vitu vya msingi usivyotakiwa kufanya wakati unaendesha magari haya ili kuongeza maisha ya gear box (Transmission Box).
 
Usipaki gari lako bila kuweka Parking Brake (hand brake)
Mara nyingi madereva wamekuwa wakipaki magari yao kwa kuweka gear leaver kwenye herufi P, bila ya kuengage Parking Brake (wengi tunifahamu kama hand brake).
 
Kama wewe ni mmoja wao tafadhali acha kufanya hivyo kwa sababu ‘Parking Pawl’, kichuma kinachoizuia gari kuondoka wakati imewekwa kwenye Park ni kidogo sana na hakijatengenezwa kwa kazi hiyo. Hivyo ikitokea mtu akaligonga gari lako kidogo kuna uwezekano mkubwa wa gari lako likaanza kutembea kama ulikuwa hujalizima. Pia kipande cha Parking Pawl kilichovunjika kinaweza kikaleta matatizo makubwa katika gear box yako.
 
Usibadili Gear ya mbele ‘D’ kwenda ya nyuma ‘R’ moja kwa moja au ya nyuma kwenda ya mbele moja kwa moja bila ya kusimamisha gari kwanza
 
Simamisha gari lako kabisa kabla ya kuamua kubadili gear ya kutoka mbele na kurudi nyuma au vinginevyo. Kufanya hivyo bila kusimamisha gari lako kutapelekea uharibifu mkubwa katika gear box yako.
 
Simamisha gari lako kabisa kabla ya kuamua kubadili gear ya kutoka mbele na kurudi nyuma au vinginevyo. Kufanya hivyo bila kusimamisha gari lako kutapelekea uharibifu mkubwa katika gear box yako.
 
Back
Top Bottom