Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mahabusu ya watoto ya mkoa wa Arusha iliyojengwa miaka zaidi ya arobaini iliyopita inakabiliwa na changamoto kubwa ya uchakavu wa majengo pamoja na miundombinu mingine muhimu hali inayotishia hali ya afya ya watoto wanaohifadhiwa humo wakikabiliwa na makosa mbalimbali.
 
Msimamizi wa mahabusu hiyo Musa Mapua anaueleza ujumbe wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi waliowatembelea watoto hao kwa lengo la kuwapelekea mahitaji mbalimbali kuwa ubovu huo wa miondombinu ikiwemo ya maji safi na taka unatishia kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko.
 
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa watoto ikiwa ni moja ya maadhimisho ya miaka arobaini na moja ya kuzaliwa kwa CCM Diwani wa kata ya kati Abdi Tojo akawakumbusha wazazi jukumu lao la malezi ili kuwaepusha watoto kuishi kwenye mazingira hayo ambayo sio salama.
 
Mahabusu hiyo kwa sasa ina jumla ya watoto kumi na watano walioingizwa kwa makosa mbalimbali ambayo mengi yanaelezwa kuchangiwa na watoto kuachwa huru wakidhurura kujitafutia mahitaji hali ambayo Mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo wa Arusha Godliving Kissila anasema wameweka utaratibu wa kuanza kuidhibiti.
 
Msanii wa muziki bongo asiyeisha vituko, Zuwena Mohamedi maarufu kama Shilole, ameweka wazi janga lililomkuta kwenye nguo aliyovaa ambayo imeonekana kuwaacha watu midomo wazi huku wakimcheka.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Shilole amesema nguo hiyo aliagiza mtandaoni, lakini matokeo yake ilikuja kumbadilikia baada ya kuvaa.
 
Kwaweli haya mambo ya kununua vitu mitandaoni yamenicost, nguo mimi nimeiona nikaagiza ikaja, nikajaribu siku ya kwanza ikanikaa vizuri tu, siku ya sherehe nikasema nivae leo ile gauni, nikavaa na ikanikaa vizuri tu, sasa balaa likaja kadri ninavoenda na yenyewe inashuka, nikasema hili sasa balaa na nishafika kwenye sherehe, ndio hivyo”, amesema Shilole.
 
Kufuatia tukio hilo Shilole amepost kwenye ukurasa wake wa instagram akisema kuwa hatokuja kurudia kuagiza nguo za mitandaoni, kuepuka lililotokea.
 
Kufuatia tukio hilo Shilole amepost kwenye ukurasa wake wa instagram akisema kuwa hatokuja kurudia kuagiza nguo za mitandaoni, kuepuka lililotokea.
 
Rais mpya wa Liberia George Weah ame kupunguza mshahara wake kwa asilimia 25 alipokuwa akilihutubia taifa kuhusu hali ya uchumi ambapo alionya kwamba nyakati ngumu zinakuja kwa vile nchi “imefilisika”.

"Hali ya uchumi ambayo utawala wangu umerithi unahitaji mengi kufanyika na kuamua,” alisema mwanasoka huyo nyota wa zamani.
 
Hotuba hiyo ni kama ilitumika kupunguza matarajio makubwa aliyokuwa nayo baada kuibuka mshindi mwaka jana kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Ellen Johnson Sirleaf.

"Nchi yetu imefilisika; serikali yetu imefilisika. Sarafu yetu inaporomoka; mfumko wa bei unapanda,” alisema Weah. "Ukosefu wa ajira ni mkubwa haijapata kutokea na fedha zetu za kigeni zimepungua sana”.
 
DAKIKA za mwisho hizi. Arsenal inakaribia kumchukua staa wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick-Aubameyang baada ya kukubali kutoa zaidi ya Pauni 55 milioni kwa staa huyo wa Gabon, lakini hapo hapo imetangaza bei ya Olivier Giroud.

Inadaiwa Chelsea inamtaka mshambuliaji huyo mrefu wa kimataifa wa Ufaransa baada ya kuchoshwa na vimbwanga vya klabu ya AS Roma ambayo inambania mshambuliaji Edin Dzeko kwenda Stamford Bridge.
 
Back
Top Bottom