Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Na sasa Arsenal imekuja hadharani na kutaka kiasi cha Pauni 35 milioni kutoka Chelsea kama kweli inamtaka mshambuliaji huyo ambaye nafasi yake Emirates imekuwa shakani baada ya kuwasili kwa Alexander Lacazette dirisha kubwa lililopita.
 
Ujio wa Aubameyang kutoka Dortmund unatazamiwa kufuta kabisa nafasi ya Giroud Emirates na staa huyo amekubali yaishe huku akitazamiwa kwenda Chelsea baada ya staa huyo kutohusishwa na Dortmund katika dili la Aubameyang kutua Arsenal.
 
Chelsea inaonekana kuchemsha katika mbio za kumpata Dzeko lakini licha ya bei ya juu ya Arsenal kwa Giroud lakini ina uhakika wa kumtumia mchezaji huyo katika mechi za Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa vile Giroud hajacheza msimu huu.
 
Hapana. Nataka Olivier abakie. Nimeshawaambia kama hakuna ambaye atakuja, basi hakuna ambaye ataondoka. Labda wachezaji wawili chipukizi watakwenda kwa mkopo kwingineko lakini wachezaji wazoefu watabakia katika kikosi labda kama kuna mchezaji mpya hatakuja,” alisema Wenger.
 
Kwa upande wa Aubameyang, endapo uhamisho wake kwenda Arsenal ukikamilika, basi Arsenal itakuwa imevunja rekodi ya uhamisho kwa mara ya pili ndani ya miezi sita baada ya kuvunja rekodi hiyo kwa Lacazette katika dirisha kubwa lililopita wakati ilipomnunua kwa dau la Pauni 52 milioni kutoka Lyon ya Ufaransa.
 
Wenger amekusanya pesa katika madirisha haya mawili ya uhamisho baada ya kuwauza baadhi ya mastaa wake kama vile Gabriel, Alex Oxlade-Chamberlain, Theo Walcott, Francis Coquelin, Alexis Sanchez huku sasa akitazamiwa kumuuza Giroud.

Arsenal pia imeendeleza mbio zake za kumchukua beki wa kati wa West Brom, Jonny Evans na kwa sasa haina upinzani katika mchakato wa kuisaka saini ya beki huyo wa zamani wa Manchester United kwa sababu wapinzani wao katika saini hiyo Manchester City wanakaribia kumnasa beki wa Athletic Bilbao, Aymeric Laporte.
 
Beki huyo anatazamiwa kutua Etihad saa 24 kuanzia sasa baada ya kusema kwaheri kwa wachezaji wenzake wikiendi iliyopita na anatazamiwa kununuliwa kwa dau la Pauni 57 milioni ambazo zipo katika kipengele cha mauzo ya mkataba wake.

Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa anatazamiwa kuwa mchezaji ghali katika historia ya City wakati huu Kocha Pep Guardiola akiwa na wasiwasi na kiwango cha nahodha wake, Vincent Kompany ambaye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara.

Guardiola pia ana wasiwasi na viwango vya mabeki wake wengine Eliaquim Mangala na John Stones na amepania kuimarisha safu yake ya ulinzi katika dirisha hili huku akiachana na safu ya ushambuliaji ambayo inaonekana kuwa moto.
 
c1fa821d66ff0d6e8720937110172205.jpg
 
Back
Top Bottom