Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

images%288%29.jpg
 
Dereva taxi mashuhuri wa Moshi mjini, Frank (35), amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kusafirisha kilo 216.3 za dawa za kulevya aina ya Mirungi.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, mtuhumiwa huyo maarufu kwa jina la "Gaucho" ataunganishwa na mshitakiwa mwenzake aitwaye Anitha Oswalid (32) aliyefikishwa kortini Januari 4.
 
Anitha ni mtumishi wa umma katika moja ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii mkoani Kilimanjaro na kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu mkazi, Aidan Mwilapwa ambaye leo alikuwa na majukumu mengine.

Mshitakiwa Frank amefikishwa mahakamani leo Jumanne Januari 30 mbele ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, Jullieth Mawole, amesomewa shitaka lake na wakili wa Serikali kanda ya Moshi, Agatha Pima.
 
Hata hivyo mshitakiwa huyo hakutakiwa kujibu chochote kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza kesi hiyo kutokana na kiwango cha dawa za kulevya alichoshitakiwa nacho.

Kesi hiyo kama zilivyo kesi za mauaji , husikilizwa na mahakama kuu isipokuwa pale kunapokuwepo kibali cha mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP).
 
Akimsomea shitaka hilo, wakili Pima amedai kuwa Desemba 19 mwaka jana, katika eneo la Majengo Kwa Mtey, washitakiwa hao wawili walipatikana wakisafirisha dawa hizo.

Kosa hilo ni kinyume cha kifungu cha 15(1)(b) cha sheria ya udhibiti wa dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.
 
Chini ya sheria hiyo inayoangukia katika makosa ya uhujumu uchumi, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya, atatumikia kifungo cha maisha jela.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 2, wakati itakapotajwa mbele ya Hakimu mkazi Mwilapwa anayeisikiliza, na siku hiyo ndipo washitakiwa wataunganishwa rasmi pamoja katika shitaka hilo.
 
Wachimbaji wanne wamefariki na mmoja yupo mahututi baada ya kuangukiwa na Ngema walipokuwa wakipakiza changarawe kwenye gari katika machimbo ya changarawe yaliyopo katika mlima Murieti katika jiji la Arusha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha leo Januari 30 kuhusu kutokea tukio hilo mchana, katika eneo ambalo ni machimbo ya muda mrefu ya changarawe.
 
Miili ya watu watatu tayari imetambulika ambao ni Yusuph Mohamed Kamwende(35) Athuman Hussein umri wake haujatambulika na Richard Kishimbo(57).

"Bado mwili wa marehemu mmoja haijafahamika na tunaomba watu kufika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru kutambua ndugu zao" amesema Kamanda.
 
Hata hivyo, ametoa wito kwa maafisa madini kwenda mara kwa mara kwenye maeneo ya machimbo ili kutazama usalama wa maeneo hayo ili kuondoa majanga.

"Pale inaonekana ngema moja ilikuwa imelegea sasa wao wakiwa wanachimba changarawe ndipo iliwadondokea na kuwafukia" amesema
 
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, John Lemanya amesema wakati watu hao wakichimba, ilisikika mlio wa kuanguka ngema na waliona wakiangukiwa.

"Wao walikuwa wameingia chini ya ngema na kuanza kukata miamba na ndipo mtikisiko ulitokea na kufanya kumeguka kwa ngema na kuwaangukia"Amesema
 
Hata hivyo hili ni tukio la pili ndani ya miaka mitatu kutokea ambapo mwaka juzi pia machimbo hayo yalifungwa baada ya kusababisha vifo kutokana na wachimbaji kuangukiwa na ngema.
 
Kamati ya Kudumu ya Kanuni za Bunge inakutana leo Jumanne kukamilisha masuala mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa kumshtaki bungeni na kumwondoa rais.

Awali kamati hiyo ilikutana Alhamisi iliyopita kujadili pendekezo la “jopo mchanganyiko” lenye wabunge, majaji wastaafu na wanasheria watakaoweza kushughulikia kwa kina mchakato wa kumshtaki rais.
 
Mchakato huu ndio unapewa uwezekano wa kutumika dhidi ya Rais Jacob Zuma, endapo atapuuza wito wa kumtaka ajiuzulu. Kilichosalia ni kukamilisha mchanganyiko wa watu katika kamati au jopo na mchakato wake kabla ya kuwasilisha ripoti kwenye kamati ya pamoja ya kanuni kisha kuisoma ndani ya Bunge la Taifa.
 
Back
Top Bottom