Huyu jamaa hapa kushoto kabisa aliyechuchumaa na koti lake jeusi utafikiri Andjul. Carba njoo ututhibitishie kama kweli ni yeye [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hivyo kama umeweza kusonga mbele kwa kuachana na mambo fulani yaliyowahi kuumiza moyo wako unayo sababu ya kujipongeza sana kwakuwa umeweza kupiga hatua kubwa ambayo imekuepusha na madhara mengi yakiwemo ya msongo wa mawazo na magonjwa mbalimbali.
8. Kama unajiheshimu na kuheshimu wengine.
Ni jambo baya sana kumdharau mwingine kutokana na shinikizo lolote kama vile umasikini, ipo kanuni rahisi sana ya maisha “usimtendee mwingine jambo ambalo usingependa utendewe pia” Kama unajiheshimu na kuheshimu wengine hakika utaheshimika pia. Hivyo kama wewe ni mmoja wa watu wanao penda kutenda haki, unayo sababu ya kujipongeza.
9. Kama hauna majivuno na ubinafsi.
Kama ilivyokuwa katika sababu iliyopita, tabia ingine unayotakiwa kuiondoa ni majivuno na ubinafsi mbele ya wengine. Kama wewe ni mtu usiyependa kujivuna na kuukumbatia ubinafsi juu ya wengine, unakila sababu ya kujipongeza.
10. Kama unaishi kwa imani.
Ingawa kuishi maisha bila hofu ni jambo gumu, unapaswa kutambua kuwa hofu inaweza kurudisha nyuma maendeleo yako mara million kuliko kitu kingine. Hivyo ishi kwa imani , usimpe hofu na mashaka maisha yako.
11. Kama ni mtu wa Maendeleo.
Muda utakajisemea kuwa umeridhika na kiwango cha maendeleo yako kimaisha, maisha yako yataporomoka , endelea kusonga mbele kila siku bila kujali kiwango cha maisha yako.
12. Kama unajipenda na kuwapenda wengine.
Kuna usemi usemao “Upendo huanzia nyumbani mwako” Usemi huu una maana gani? Kama huwezi kujipenda mwenyewe utawezaje kumpenda mwingine,
taswira gani ya upendo utawaonyesha wengine? Ni vipi unaweza kutoa kitu usichokuwa nacho? Majibu ya maswali hayo yatakupa kipimo halisi cha hali ya upendo wako
Huyu jamaa hapa kushoto kabisa aliyechuchumaa na koti lake jeusi utafikiri Andjul. Carba njoo ututhibitishie kama kweli ni yeye [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.