Wachanganuzi wanaamiini kuwa jinamizi la Al Shabab ni gumu kuliangamiza..
Hassan Sheikh, ni mchambuzi wa masuala ya usalama anasema, 'Kwa sababu ni wapiganaji, wanaweza kupenya kirahisi katika maeneo ya umma na ya kibinafsi, na wana athari kubwa katika mfumo wa jamii kisiasa, kiuchumi na kijamii.
'Muhimu zaidi ni kuwa walisababisha uoga, na uoga huu huwasaidia kwani ni vigumu sana kuwakamata au kuwashinda'.
Mapema wiki hii, mahakama kuu ya Somalia ilimpata na hatia mshukiwa mmoja wa mashambulio hayo na kumhukumu kifo, huku mwengine ambaye hakuwa mahakamani akihukumiwa kifungo cha maisha.
Barabarani, kikosi maalumu cha jeshi kimeimarisha ukaguzi wa magari haswa nyakati za jioni; huku magari karibu yote yakisimamishwa na kukaguliwa vikali pamoja na abiria.
Wakazi wanatumai kwamba hatua hizi zitaweza kurejesha matumaini yao ambayo kwa sasa yako gizani.