Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4) Ni kwasababu ya Upendo tuna ujasiri hata siku ya hukumu.
“Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.” 1 Yohana 4 :17
 
6) Upendo husamehe.
“ Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.” Wakolosai 3 :13
 
7) Kwasababu ya Upemdo tunaweza kuvumiliana.
“Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;… huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.” 1 Wakorintho 13 :4, 7
 
8) Upendo una nguvu ya kuvuta watu kwa Mungu.
“katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.” Tito 2 :7-8
 
9) Upendo hutupilia mbali hofu na woga.
“Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.” 1 Yohana 4 :18
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…