Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kinyume na fikra za watu wengi, kupanda mlima Kilimanjaro haihitaji mazoezi mengi sana. Kilimanjaro Guide inaeleza kwa nini wanawake na wanaume wenye umri kati ya 40 na 60 wanafanikiwa kupanda mlima huu zaidi ya vijana wenye umri kati ya 20 na 30. Ni kwa vile vijana wanaopanda mlima wanaanza na kasi sana na wanaishia kuchoka mapema, badala ya kwenda kidogo kidogo. Inashangaza eh?
 
1. Tembea, tembea na tembea zaidi

Hii ni muhimu sana kama unataka kufika juu kabisa. Utatembea sana kliko vitu vyote ukipanda mlima huu kwa hiyo, anza kutembea sana katika mazoezi yako ya kupanda Kilimanjaro.
 
Watu wengi wakiwa wanajiandaa kupanda Kilimanjaro wanasahau kwamba unafika kila kituo kwa kutembea masaa 5 au 8 kwa siku. Kawaida inachukua siku 6 au 8 kufika kileleni na kwa hiyo, utakuwa unatembea kwa masaa 5 au 7 kwa siku. Hakikisha unajiandaa kwa hii.
 
2. Chagua njia ya kupanda kabla

Ni kawaida kuwa na hamu kufika kwenye kilele ya Afrika, ila, inabidi ujihami na ukumbuke kwamba hakuna faida kuharakisha.
 
Kuharakisha inaweza ikakuletea madhara zaidi. Watu wanaotaka kupanda mlima ndani ya siku 4 au 5 wanaweza wakaamua kutumia njia ya kasi zaidi.Ila, wanasahau kukumbuka kwa mwili inahitaji muda wa kujizoesha kwa viwango vya chini vya oksijeni, kadri unavyopanda. Hii ndio maana watu wengi wanaishia kuugua kadri wanavyopanda mlima na hivyo, kushindwa kuupanda. Badala yake, pitia njia zote na pia soma maoni ya watu juu ya njia hizi.
 
Utapata mtazamo wa njia itakayokufaa ili upande mlima kwa furaha na mafanikio. Kulazimishwa kurudi inasikitisha, hasa ikiwa kwamba afya yako ni nzuri ila hukuwa na subira na hivyo ukakosea kwa kutumia njia ya kasi na ukaishia kuumwa. Kumbuka, haraka haraka haina Baraka.
 
Utapata mtazamo wa njia itakayokufaa ili upande mlima kwa furaha na mafanikio. Kulazimishwa kurudi inasikitisha, hasa ikiwa kwamba afya yako ni nzuri ila hukuwa na subira na hivyo ukakosea kwa kutumia njia ya kasi na ukaishia kuumwa. Kumbuka, haraka haraka haina Baraka.
 
3. Maji ni rafiki yako wa karibu!

Hupendi kunywa maji? Anza kujizoesha kunywa! Kuwa na hidarati ni lazi kama una matumaini ya kufika mbali. Mwili wako unakosa hidarati kwa kasi zaidi kwa sababu ya mwinuko na hii inaweza ikasababisha usikia kizunguzungu au upate maumivu makali ya kichwa.
 
Watu waliofanikiwa kufika kileleni na kushuka kwa usalama wanapendekeza unywe lita 5 za maji kwa siku. Hii inaweza ikaonekana kuwa ngumu kufanya, ila ni lazima kama unatarajia kufika kileleni.
 
4. Fanya mazoezi kwenye sehemu zenye milima na uongeze uzito

Ukiwa unapanda mlima Kilimanjaro, utakuwa umebebabegi nzito na utabidi upande milima mikali pamoja na begi hiyo.
 
Njia moja ya kujiandaa kwa hii nikutembea kwenye sehemu yenye milima mikali karibu na nyumbani, ukiwa umevaa begi hiyo. Kumbuka kuanza na mlima isiyokali sana ila ukali uongezeka kadri unavyo fanya mazoezi. Pia, ongeza uzito kwenye begi kadri unavyofanya mazoezi.
 
5. Kumbuka lengo lako

Unajua kwamba mwanamke mwenye umri zaidi aliyewahikupanda Kilimanjaro alikuwa na miaka 86? Angela Vorobeva alithibitisha kwa watu wengi waliokuwa na wasiwasi wa kupanda mlima huu kwamba mtu yoyote anaweza kuupanda. Kuwa na afya bora sio kila kitu.
 
Unavyopanda Kili – jina la kifupi la Kilimanjaro ilyopewa na wakazi wa hapo – ni lazima ukumbuke sababu yako ya kuupanda na utakavyojisikia ukikamilisha lengo lako.
 
Hii itakusaidia sana ukijisikia kukata tamaa. Tunatumaini kwamba sababu yako ya kupanda Kili ni zaidi ya kuweza kujisifia kwamba umepanda mlima Kilimanjaro.
 
6. Vaa kwakuzingatia mazingira

Ni lazima uwe na mavazi sahihi kama hutaki kuganda au kupata ugonjwa wa mwinuko. Utafiti mkubwa wa glovu bora, begi bora, viatu vizuri na hata chupi zinasaidia kuhakikisha kwamba unajisikia vizuri kiasi ukipanda na ukishuka.
 
Hutaki kuwa na wasiwasi juu ya miguu baridi, mdomo uliokatika au kutokuwa na betri kwa ajili ya tochi, ukiwa umeshachoka sana. Rahisisha maisha yako kwa kuwa na mavazi sahihi.
 
7. Jiandae na maisha ya kawaida sana

Isikushangaze kwamba kati ya hizo siku 6 au 8 utakazo kuwa unapanda mlima, hutaweza kuoga. Wanawake, naomba msahau swala la vipodozi kabisa!
 
Watu wengine wanapata wakati mgumu kwenye maisha ya kambi. Kabla ya kwenda kupanda mlima, jaribu kupanga safari ndogo ya kambi ili upate mazoefu zaidi ya kambi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…