Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mabata mzinga au mapiru (kwa Kiingereza anaitwa turkey) ni ndege wakubwa wa jenasi Meleagris, jenasi pekee ya nusufamilia Meleagridinae katika familia Phasianidae. Ndege hawa ni wakubwa kabisa wa Phasianidae.
 
Anafanana kidogo na bata, ana manyoya ya kahawia,kichwa kisicho na manyoya na shingo yenye ngozi ya makunyazi isiyo na manyoya. Kichwa chao hakina manyoya na kina rangi nyekundu, pinki au ya kijivu. Manyoya yana rangi nyeusi imetayo yenye madoa.
 
Spishi

Meleagris gallopavo, Bata Mzinga Mwitu (Wild Turkey)
Meleagris g. gallopavo f. domesticus, Bata Mzinga Kaya ( Domesticated Turkey)
Meleagris ocellata, Bata Mzinga Mkia-madoa (Ocellated Turkey)
 
Spishi za kabla ya historia

Meleagris californica (Mwisho wa Pleistocene ya Marekani ya kusi-magharibi)
Meleagris crassipes (Mwisho wa Pleistocene ya Marekani ya kusi-magharibi)
Meleagris sp. (Mwanzo wa Pliocene ya Bone Valley, MMA)
Meleagris sp. (Mwisho wa Pliocene ya Macasphalt Shell Pit, MMA)
 
Mbizi au michemba ni ndege wa maji wa jenasi Anhinga, jenasi pekee ya familia Anhingidae. Wana shingo refu na domo refu lenye ncha kali na makali ya menomeno. Huzamia chini ya maji ili kuwakamata samaki wakiuliza domo lao kama mkuki. Huzaa kwa makoloni na hujenga tago lao la vitawi mitini au kwa matete.
 
Spishi za kabla ya historia

Anhinga subvolans (Mwanzo wa Miocene ya Thomas Farm, MMA) – zamani iliainishwa katika Phalacrocorax
Anhinga cf. grandis (Kati ya Miocene ya Kolombia mpaka mwisho wa Pliocene ya Amerika Kusini)
 
Anhinga sp. (Kati ya Miocene ya Mátraszõlõs, Hungaria)
Anhinga fraileyi (Mwisho wa Miocene mpaka mwanzo wa Pliocene ya Amerika Kusini)
Anhinga minuta (Mwisho wa Miocene/mwanzo wa Pliocene ya Amerika Kusini)
 
Anhinga pannonica (Mwisho wa Miocene/mwanzo wa Pliocene ya Tataruş-Brusturi, Hungaria na Libiya, Tunisia, Pakistan na Uthai)
Anhinga grandis (Mwisho wa Miocene mpaka mwisho wa Pliocene ya MMA)
Anhinga malagurala (Mwanzo wa Pliocene ya "Charters Towers", Australia)
 
Anhinga sp. (Mwanzo wa Pliocene ya "Bone Valley", MMA)
Anhinga hadarensis (Mwisho wa Pliocene/mwanzo wa Pleistocene ya Afrika ya Mashariki)
Anhinga sp. (Mwanzo wa Pleistocene ya Coleman, MMA) – labda ni moja na Anhinga sp. "Bone Valley"
 
Koikoi ni ndege wakubwa wa jenasi Ardea katika familia ya Ardeidae wenye miguu mirefu na domo refu na nyembamba. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Ndege hawa wana rangi nyeupe, kijivu na nyeusi. Spishi zenye rangi ya kahawiachekundu huitwa pondagundi pia
 
Spishi nyingine nyeupe kabisa inaitwa msuka. Zamani ilikuwa imeainishwa ndani ya jenasi Egretta. Koikoi hupenda kula samaki lakini hula wanyama wadogo pia, kama vyura, mijusi na nyoka. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti. Jike huyataga mayai 2-6.
 
Yangeyange ni ndege wakubwa wa jenasi mbalimbali ya nusufamilia Ardeinae katika familia Ardeidae wenye miguu mirefu, shingo ndefu na domo refu na jembamba. Hupinda shingo yao wakiruka angani.
 
Ndege hawa ni weupe au weusi au rangi hizi mbili (pengine kijani au buluu). Spishi nyingine huitwa kulasitara au dandala. Yangeyange wengine hupenda kula samaki, wengine hula wadudu na wanyama wadogo kama vyura na mijusi. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti, matete au mafunjo.
 
Keremkerem ni ndege wa familia ya Meropidae. Wana rangi maridadi na mwili wao ni mwembamba. Domo lao ni refu na jembamba na mkia wa aina nyingi ya keremkerem una mileli mirefu katikati.
 
Kolokolo ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wanafana na videnenda lakini mkia wao ni mrefu zaidi na wana rangi kali zaidi: kahawia, kijivu au kijani mgongoni na nyeupe, njano na/au nyekundu chini na pengine kichwani na mbawani. Spishi nyingi zina mkufu mweusi kidarini. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika misitu na mapori. Hula wadudu. Hulijenga tago lenye kuba ya manyasi, majani na/au vigoga katika kichaka. Jike huyataga mayai 3-5.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…