Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania.

Kusini mwa ziwa unatoka Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.

Kijiolojia ziwa ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.
 
Eneo la Ziwa

Eneo la ziwa ni km² 29,600. Sehemu kubwa ni eneo la Malawi, robo ya kusini-mashariki ni eneo la Msumbiji, robo ya kaskazini-mashariki ni eneo la Tanzania. Lakini kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba mpaka uwepo katikati kufuatana na desturi za kimataifa.
 
21479676_1795843550444976_7460439247774810112_n.jpg
chupa hizo zimetoka kwa friji....
 
Sababu ya mzozo ni utaratibu wa kikoloni. Wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kulikuwa na mpaka wa kimataifa kaskazini mwa ziwa. Baada ya mwaka 1919 Uingereza ilitawala Tanganyika pamoja na Malawi (Nyasaland). Kwa kusudi la kurahisisha utawala mambo yote yaliyohusu ziwa yaliwekwa chini ya serikali ya kikoloni ya Nyasaland.
 
Baada ya uhuru Malawi ilijaribu kutumia desturi hizo kama haki yake ya kitaifa. Polisi yake ilijaribu kutawala wavuvi na feri za Tanzania ziwani. Mzozo huu ulisababisha risasi kufyatuliwa baada ya uhuru. Hadi leo hakuna mapatano rasmi lakini nchi zote mbili zinaendelea bila kutumia nguvu. Hali halisi Malawi imeheshimu dai la Tanzania haijasumbua tena wavuvu au feri za jirani ndani ya robo ya kaskazini-mashariki ya ziwa.
 
Back
Top Bottom