Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

cea1eb632be32827f4b803f5d148e351.jpg
 
NJIA BORA YA KULITAZAMA NA KULITENDA JAMBO. . SIKU MOJA Baba akiwa anajisomea gazeti, binti yake mdogo alikuwa akimtaabisha kwa michezo yake ya hapa na pale. Ili kumtuliza, alichukua karatasi ambayo kwa mbele ilichorwa ramani ya dunia, akaichanachana vipande vitano na kuvichanganya. Kisha akampa binti yake, akimtaka akakae chumbani na kuviunganisha ili kuurudisha mchoro wa ramani. Alikuwa na hakika kwamba ingemgharimu siku nzima kuupata mchoro ule. . Muda mfupi baadaye, binti alirejea na karatasi yake mkononi, akiwa amepatia kuupanga upya mchoro wa ramani kwa vipande vya karatasi vilivyochanwa. Kwa Baba alipomuuliza bintiye, ilikuwaje hata akafanikiwa kwa haraka kuipanga upya ramani ile. . Binti alijibu, "Baba, wakati unaichana hiyo ramani, nyuma ya karatasi hiyo kulikuwa na mchoro wa picha ya mtu. Kwa hivyo, nilichokifanya niliipanga vizuri ile picha ya mtu na nilipoigeuza nyuma tayari ramani ikawa imejipanga yenyewe." . Baada ya kumstaajabisha baba yake, binti alikimbia zake nje kwenda kucheza. . . FUNZO: Siku zote, kuna upande wa pili wa utatuzi wa tatizo pale upande mwanzo unapokuwia mgumu. Kwahiyo, ukumbwapo na tatizo au changamoto, na likakushinda kutatua. Usikate tamaa, hakika iko namna nyingine ya kulitazama, kulichunguza jambo lako, ili kulitatua kwa njia mbadala
 
KISA CHA MZEE, NA MCHE WA MZABIBU. . Akiwa matembezini, siku moja Mfalme Ghally alimwona mzee mmoja kikongwe akipanda mche wa mzabibu bustanini. . Tukio hilo, kiasi lilimstaajabisha Mfalme, ikabidi amsogelee na kumuuliza, "Mzee, kwanini hasa unahangaika kupanda mche wa mti huu ambao utachukua miaka mingi mpaka kukua, na pengine wewe utakua umekwishakufa kabla hata ya kuonja matunda yake?". . Huku ametabasamu mzee alijibu, "Ooh, waliipanda mizabibu wazee waliotangulia kabla yetu na zabibu tukala sisi. Sioni ubaya nami kuupanda mzabibu huu kwa faida ya vizazi vijavyo.". . Jibu lile lilimsisimua sana mfalme. Kwa hakika hakutaraji kuona katika dunia ya leo wangalipo watu wanaojitolea kufanya jambo kwa ajili ya manufaa ya wengine. Kwa furaha, Mfalme aliwaamuru wafuasi wake wampe pesa (Dinari miamoja) yule mzee kama pongezi. . Mzee alizipokea pesa kwa furaha huku akijisemea kwa sauti, "Maajabu gani haya! yaani mzabibu wangu umeanza kuzaa matunda mwenyewe ningali hai!". . Majibu ya mzee yalizidi kumstaajabisha mfalme. Ilimdhihirikia wazi kwamba ni kweli mzee amepata matunda (faida) ya mti wake kipindi mwenyewe akiwa hai kitu ambacho hakutazama kutokea. Kwa furaha, Mfalme aliwaamuru wafuasi wake wamwongeze pesa nyingine yule mzee. . Mzee alipozipokea pesa zile, aliinua macho mbinguni huku akijisemea, "Maajabu juu ya maajabu. Pamoja na kwamba haujakuwa, lakini mzabibu wangu umezaa mara mbili kwa mwaka, tena mwenyewe nikiwa hai!". . Mfalme alipigwa butwaa akiyatafakari maneno ya mzee kwa kusadiki anenayo. Ni kweli kwamba, kwa malipo mara mbili aliyompa mzee kama pongezi, ni sawa kabisa kwake na kuvuna mara mbili kwa mwaka kwa zao ambalo hakutarajia kuona hata ukuaji wake. . Baada ya kujifikiria, Mfalme aliwasogelea wafuasi wake na kuwanong'oneza, "Mpeni tena Dinari mia nyingine halafu tuondoke haraka asije akasema tena neno zuri mpaka tukaishiwa pesa hapa!". . SOMO: Katika maisha kufanya jambo jema kwa uzalendo hata kama lengo ni kuwanufaisha wengine, mwisho wa siku yako mavuno yatakayokufikia kwa njia usiyoitarajia.
 
MZEE mmoja aliona nge akitapatapa kuzama kwenye maji. Imani na roho ya kusaidia ikamjia, akaingiza mkono majini ili kumhami. Alipomgusa tu, nge akamgonga. Maumivu aliyoyapata, alijikuta akitoa mkono bila kumuokoa. . Pamoja na maumivu ya sumu ya nge, mzee alipotupa macho tena majini, alimwona nge akizama na kutapa. Haraka aliingiza mkono ili kumsaidia. Na kama awali, nge akamgonga tena na kumwachia maumivu makali. . Kijana aliyekuwa amesimama kando, alimuuliza mzee: "Kumradhi mzee, naona kama utadhurika bure. Hivi huoni kila unapojaribu kumsaidia, naye anazidi kukugonga?". . Mzee alijibu, "Uhalisia wa nge ni kugonga, uhalisia wangu kama mwanaadamu ni kusaidia. Uhalisia wangu wa kusaidia, hauwezi kubadilika kama ambavyo uhalisia wa nge wa kugonga usivyobadilika.". . Punde, mzee alichukua kipande cha mti, akakitumia kumuopoa yule nge na kumtoa nje ya maji. Kijana akaandoka kichwa chini, mikono nyuma. . FUNZO: Kamwe usijibadili uhalisia wako. Ukifanya ihsani ukalipwa nuksani, usibadilike. Badala yake, chukua tahadhari kisha badili mfumo wako wa kusaidia. Hutokea kipindi mtu akakudhuru si kwa makusudi, bali kwa mapungufu yake ya kimaumbile. Kwahivyo, kulipizia uovu ni kujidhulumu nafsi na kujishushia hadhi. . Kama lipo ulilojifunza,
 
RAIS wa zamani wa India, Dr. AbdulKalam, alipata kusimulia: "Siku moja usiku, nilipokuwa mtoto, nakumbuka kumwona mama yangu akituletea chakuka mezani nikiwa na baba. Mama aliniwekea sahani ya chapati, huku akimwekea baba sahani yenye chapati iliyoungua. . Nilijaribu kumtulizanishia macho baba ili kuona atafanyeje. Baba alianza kula chapati ile iliyoungua huku akiniuliza kuhusu maendeleo yangu shuleni. . Sikumbuki nilichomjibu, ninachokumbuka ni kumsikia mama akimtaka radhi baba kwa kuunguza chapati. Na kamwe sitasahau majibu ya baba pale alipomjibu mama kwa kumwambia, 'Oh, usijali mpenzi. Huwa hupenda pia chapati za kuungua.'. . Baadaye usiku huo, nilipokwenda kumbusu baba na kumtakia usiku mwema, ndipo nilipomuuliza kama ni kweli hupendelea chapati za kuungua. . Alinikumbata mikoni mwake na kuniambia, 'Leo, mama yako alitingwa mno na majukumu ya kazini hata akawa amechoka sana, ndipo akaunguza chapati. Lakini, kwa bahati, chapati iliyoungua haiwezi kumuumiza mtu kiasi cha kumchoma moyoni, walakini maneno makali yanaweza kumuumiza. Hivyo, sikuwa na sababu ya kumshutumu kwa maneno makali. Hata kama sipendi chapati za kuungua, ila kumjibu vile kumemfanya awe huru. Unajua maisha nayo hayako kamili kama tusivyo kamili sisi wanaadamu. Kwahivyo, ili kudumisha furaha na kuboresha mahusiano na maelewano baina yetu, ni lazima tujifunze kuyakubali na kuyakabili mapungufu yetu - Chapati za kuungua hazidumu milele, zikishasagika tumboni utakwenda kuzitoa msalani. Lakini, maneno makali huacha majeraha ya kudumu moyoni.'.
 
HAPO KALE kuna mzee alisambaza uzushi kwamba, kijana mmoja ambaye ni jirani yake alikuwa mwizi. Kama ilivyo kawaida ya uzushi, huvuma na kusambaa kwa kasi ya upepo. Matokeo yake, kijana alitiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani. . Kijana aliachiwa huru baada ya ushahidi kutokukamilika, na hapo ndipo alimfungulia mashitaka yule mzee kwa kumtuhumu kimakosa na kumchafulia jina lake. . Mahakamani, mzee alimwambia Jaji: "Yale niliyoyasema juu ya kijana huyu yalikuwa maoni yangu tu, na hayamdhuru yeyote.". . Baada ya kumsikiliza mzee, Jaji alimwambia: "Sawa, nimekusikia. Sasa nakuagiza, andika hayo maelezo yako yote ya utetezi kwenye karatasi. Kisha, uichane hiyo karatasi vipandevipande, na utakopitoka mahakamani upite mtaani ukirusha kipande kimojakimoja cha karatasi hadi utakapofika kwako. Kesho mrejee mahakamani kwa ajili ya kusikiliza hukumu.". . Siku iliyofuata, Jaji alimwambia yule mzee: "Kabla sijaanza kutoa hukumu, itakubidi upite ukikusanya vile vipande vya karatasi ulivyovisambaza jana.". . Kwa wahaka, mzee alijibu, "Sitaweza kufanya hivyo. Upepo ulikwishavisambaza na siwezijua wapi pa kuvipatia tena.". . Jaji alijibu haraka: "Vivyo hivyo, uvumi wa wizi uliomshutumu jirani yako, umesambaa kila kona kiasi cha kumwondoshea heshima na hadhi yake katika jamii. Na hakuna namna ya kuweza kuyarejesha kinywani mwako maneno yote uliyoyasema dhidi yake bila ushahidi.". . FUNZO: Ni jukumu la kila mmoja kuudhibiti mdomo wake kutosema maneno yasiyo ushahidi, ili baadaye usijekuwa mtumwa wa maneno yako mwenyewe.
 
KISA CHA MZEE NA WAHAMIAJI WAWILI. . Kuna masimulizi kuhusu mzee mmoja mwenye busara sana aliyekuwa amekiti kizingitini nje ya nyumba yake. Mara alitokea msafiri na mabegi yake, baada ya kusabahiana aliuliza: "Samahani mzee, naomba kujua ni aina gani ya watu waishio hapa kijijini, ninatazamia kuhama huko nitokako na kuhamia hapa!". . Mzee mwenye busara alijibu kwa kuuliza: "Kwani ni kuna aina gani ya watu huko utokako?". . Msafiri akajibu, "Huko kumejaa watu jeuri, viburi, mafidhuli na wenye majigambo.". . "Ooh, pole kijana. Hata hapa, kijiji hiki kimejaa watu wa namna hiyo." Mzee alijibu. . "Aah, bora nirudi hukohuko; aheri ya zimwi likujualo, halitakula likakumaliza," Kijana alijibu huku akitokomea na mabegi yake. . Haikuchukua muda tangu kuondoka kwa msafiri huyo, mara akatokea tena msafiri mwingine na mabegi yake. Alipomfikia yule mzee, baada ya salamu, naye aliuliza swali kama la yule msafiri wa awali. Baada ya mzee kumjibu kwa kuulizia aina ya watu wa huko atokako, kijana alijibu, "Huko nitokako, watu ni wema na waungwana; wakarimu wenye maadili mema.". . "Ooh, vizuri. Kijiji hiki pia, watu wema na waungwana kama wa huko utokako, wamejaa pomoni." Mzee alijibu huku akiwasha sigara yake na kuendelea kuteketeza mapafu taratiib. . Kwa bashasha na taadhima, kijana akashusha mabegi yake na kuingia rasmi kijijini hapo. Lakini, unaweza kujiuliza ni kwa busara gani hasa, hata mzee yule akatoa majibu tofauti kwa wasafiri wawili waliouliza swali lenye kufanana? Ni rahisi tu, katika maisha, huwa tunavitazama vitu si kwa namna vilivyo bali kwa namna tulivyo sisi. Kama ilivyo rahisi kwa mja mwema kuwatazama wenziye kwa jicho la wema, vivyo hivyo kwa muovu kuwatazama wengine kwa jicho baya. Kama unawaona watu wako ni wabaya sana, basi jitazame moyoni mwako, pengine hivyo ndivyo ulivyo wewe ndani ya moyo wako. .
 
TAZAMA AKILI YA PAKA Paka akialikwa sehemu akaambiwa kuna Mouse (Panya), akishaona na kijimkia chake, mate yanamtoka, anawaza kula tu. Kumbe Mouse inaweza kuwa ya kompyuta, na mkia wake ukawa ni waya tu. . Epuka akili za paka.
 
UKUMBUKWE KWA LIPI? Takribani miaka mia moja iliyopita, mtu mmoja alikuwa akisoma gazeti litokalo kila asubuhi. Kwa mshangao na wahka mkubwa, aliona kwenye gazeti hilo, jina lake likiwa limechapishwa katika safu ya Tanzia. (Tanzia ni wasifu wa mtu aliyekufa). Gazeti hilo la kila asubuhi, lilichapisha taarifa ya kifo cha mtu mwingine, huku jina la mtu huyo likichapishwa kimakosa. Awali, alipatwa na mshituko mkubwa; akijiuliza, hivi nimekufa kweli, au? Na aliporejewa na utulivu wa nafsi, fikara ya pili ikawa ni kuona namna alivyozungumziwa na watu waluoamini kuwa amekufa kweli. . Tanzia katika gazeti hilo ilisomeka kama hivi: "Mfalme wa milipuko afariki dunia.", huku sehemu nyingine ikisomeka, "Alikuwa ni mfanyabiashara wa kifo!". Kimsingi, mtu huyu alikuwa ni mvumbuzi na muuzaji mkubwa wa milipuko (Mabomu), ambayo hutumiwa kupigania sehemu mbalimbali duniani na kupelekea vifo. Kwa hivi, alipoyasoma maandishi "Mfanyabiashara wa kifo" alitahayari na kujiuliza, "Je, hivi ndivyo nitakumbukwa pindi nitakapokufa kiukweli?". . Baada ya kichwa chake kutaabishwa na fikra juu ya kadhia hiyo, mwishowe alihitimisha mjadala kwamba, hiyo haikuwa njia bora ya kukumbukwa na jamii. Basi tangu siku hiyo, alijitanibu na biashara hiyo, huku akipambana kwa jino na ukucha kuitangaza amani, kwa kauli na vitendo. Mtu huyu aliitwa Alfred Nobel, ambaye leo hii, dunia inamkumbuka kwa ile tuzo kubwa na mashuhuri duniani ya amani ya Nobel (Nobel Prize). . Kama ambavyo Alfred Nobel, baada ya kubahatika kuona utajo mbaya wa jina lake ukisababishwa na mambo afanyayo maisha ni, akajutia na kuazimu kubadilika kabisa na hatimaye kuacha alama na heshima kubwa duniani, nasi tufanye kama yeye. Tusingoje bahati ya kusikia watakavyo tuzungumza jamaa zetu baada ya kutawafu kwetu, bali tujiandae sasa. . Ukifa utaacha hisia gani? Utakumbukwa kwa lipi? Ni upi utakuwa utajo wako? Utakumbukwa kwa upendo na heshima, au kwa uovu na udhalimu? Watu watahuzunika kukukosa, au watashukuru ukiondoka?.
 
Back
Top Bottom