Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

7dfb01b80b720b813a28351d318ae6a1.jpg
 
UNAWEZA KUACHA 'FURSA' NA KUSAIDIA? Kuna kipofu alikuwa ameketi kando mwa barabara, kwa bahati akasikia mchakato wa nyayo za mtu akipita, akasimama na kuanza kuita kama anayehitaji msaada: "Habari! Habari ndugu!" Bwana aliyekuwa akipita, akaitikia salamu na kumsogelea karibu: "Salama ndugu, kwema?" "Kwema ndugu," kipofu alijibu huku akitoa pesa mfukoni na kumkabidhi mzee, "tafadhali, nina shilingi elfu mbili hapa, kuna mtu amenipa msaada, naomba unisaidie kuichenji." Yule bwana, kuangalia vizuri mkononi mwa kipofu, akaona si shilingi elfu mbili, ni dola 100. Akaangaza huku na kule kama kuna mtu anamwona kisha akaipokea. Akaingiza mkono mfukoni, akatoa chenji ya shilingi elfu mbili na kumpa kipofu kisha akaondoka na ile dola mia. Bwana mkubwa aliona kama nyota ya jaha imemwangukia, hakumtazama kipofu yule kwa jicho la msaada. Badala yake, akatumia mwanya huo kumdhulumu. Ikawa hivi: yule bwana kabla hajafika mbali, akashangaa kumwona yule kipofu akimjia mbio na kumsimamisha. Kwa hofu na mashaka, akasimama. Kipofu alipomfikia, akavua miwani yake myeusi na kumwambia: "Samahani bwana, mimi siyo kipofu; ninafanya utafiti kuona ni watu wangapi wana uungwana wa kumsaidia mtu dhaifu - hata kama hawaonekani hadharani, na wangapi wana ushenzi wa kutatumia udhaifu wa mtu ili kumdhulumu - wakidhani hawaonekani. Umefeli mzee!" Uso ukiwa umemshuka kama mbuzi, yule bwana akatoa ile noti ya dola mia na kumrudishia mwenyewe huku akisema: "Samahani kaka, ni hali ngumu tu tulizonazo." Kijana akachukua pesa yake na kumwonesha yule bwana upande wa pili wa barabara. Huko walikuwapo watu kama watano hivi na kamera zao, wakirekodi video ya hilo tukio zima. Nilipoona video ya mkasa huu, nilijihisi aibu utadhani mimi ndiye yule bwana. Je, ungekuwa wewe ungefanya nini?
 
USIHUKUMU KWA HISIA. WAKIWA ndani ya treni, kijana mmoja mwenye takribani miaka 23 alisimama dirishani akitazama nje na kupaza sauti: "Baba, tazama huku, miti inarudi nyuma yenyewe." Baba alitabasamu, huku abiria wengine wakiangua vicheko vya haja, kuona kijana wa umri ule, akishangazwa na jambo la kipuuzi namna ile. Kabla hawajatanabahi, kijana alipaza tena sauti: "Heee! Baba, tazama na mawingu yanavyotufuata kwa kasi!" Baada ya abiria kuamini kwamba, kijana yule alikuwa na matatizo ya akili, mmoja alijaribu kumshauri baba wa kijana: "Sidhani kama imeshindikana kumtibu. Kwanini usitafute daktari mzuri?" Akiwa ametabasamu, baba alijibu: "Nimeshatafuta, na hapa ndo tunatokea hospitali tulikolazwa kwa miezi mitatu sasa. Kijana wangu alizaliwa kipofu, ni juzi tu ndo amewekewa hayo macho na kuanza kuona. Hivyo, kila kitu kwake ni kigeni machoni." Abiria wote wakapigwa butwaa. Kila aliyefikiri kwamba kijana alikuwa na matatizo ya akili, alifadhaishwa na majibu yale. Kimsingi, kila umuonaye tofauti hapa duniani, huwa na sababu zake za kuwa hivyo. Usimhukumu mtu kabla hujajua uhalisia wa mambo.
 
Back
Top Bottom